Meno anayotumia mbwa kucheza nawe ndio hayo yatakayotumika kukuuma ukimkanyaga mkia

Meno anayotumia mbwa kucheza nawe ndio hayo yatakayotumika kukuuma ukimkanyaga mkia

Street brain

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2022
Posts
584
Reaction score
767
Wazee wanasema "Meno anayotumia mbwa kucheza na wewe ndio hayo hayo yatakayo tumika kukuuma utakapo mkanyaga mkia".

Waweza kuumizwa na mtu ambaye unampenda mnoo mpaka ukashangaa na kujiuliza hivi ni huyu huyu kweli amenitendea hivi?

Kile unachokipenda sana chaweza kukuumiza sana vile vile. Usimue mbwa, alikuwa anatetea mkia wake kwasababu ya maumivu uliosababisha pengine bila ya wewe kujua.

Mtu mwenye nguvu sio yule anayepigana na kila mtu bali ni yule mwenye uwezo wakuzishinda hasira zake😋* Pocco

Hivi ukiiba ngoma ya raisi utaenda kuichezea kijiji gani ili asijue?😝eti ni kweli Moshi wa nyama inayochomwa huwa hauumizi macho ya mtu mwenye njaa?😝🏃🏾‍♂️
 
Umetumia code sana kufikisha ujumbe wako kwa hadhira.

Tunajua kuna watu wanalipwa mishahara kwa kazi ya kumshauri Mhe. Rais, hivyo wamshauri kwa hekima na kutanguliza mslahi ya Nchi.

Ila pamoja na hayo ni muhimu Rais akajua Watanzania wa mwaka 1961 sio hawa wa 2023
 
Usinigombanishe na rais wangu 🤣🤣🤣
 
Kuwa na amani Mkuu, Rais hawezi kukuchukia ukimkosoa kwa staha kama hivyo ulivyoandika.

Sisi Waswahili tunasema "Boliti moja haijengi Nyumba"

Tushirikiane kuifanya Tanzania Kubwa tena Duniani (Makes Tanzania Great Again - MATAGA)
Waoooh!!!🥰🥰 Mataga
 
Wewe ni mbeambea,unaandika vitu kama gwiji la usogodaji,kungwi uliekosa shipa la mdomo!. Huna tofauti na lidada lenye kiuno mbelembele kama au basi...
 
Wewe ni mbeambea,unaandika vitu kama gwiji la usogodaji,kungwi uliekosa shipa la mdomo!. Huna tofauti na lidada lenye kiuno mbelembele kama au basi...
Huenda reply yako haihusiani na jumbe yangu
 
Back
Top Bottom