meno yana achia yanaacha uwazi kadri siku zinapoenda naombeni msaada

meno yana achia yanaacha uwazi kadri siku zinapoenda naombeni msaada

candlyn

Member
Joined
Dec 28, 2013
Posts
16
Reaction score
3
habar zenu wana jm forum, na matatizo ya kuachia kwa meno yana acha njia au uwazi kadri siku zinapoenda, na hili tatizo sio mimi tu hadi dada yangu wa tumbo moja pia meno yako hivyo hivyo mimi ndyo yanaanza yeye ndyo yameacha uwazi kama katoa jino. Naomben msaada jamn nifanyaje au kuna dawa maalamu
 
Maelezo uliyotoa ni kidogo sana hivyo inakuwa vigumu kukushauri kikamilifu. Dalili ulizokuwa nazo inawezekana kuwa taya (jaw) linaenaendelea kukua hivyo kusababisha gap katika meno yako. Hizo ni dalili za ugonjwa wa kuwa na vichochezi vingi vya ukuaji (growth hormone) au kwa lugha ya kitaalam hyperpituitarism. Kama miguu yako na mikono yako ina dalili za kuongezeka ukubwa basi inaweza kuwa hilo ndio tatizo. Nenda uonane na daktari wako wa meno akuchunguze zaidi.
 
Mkuu isije kuwa ni dalili za mwanya hizi,sisi wenzio wamasai huwa namesa ngorotiki kisha nang'oa kabisa jino ya mbele wewe inatokea natural unajisikia unyonge?
 
Back
Top Bottom