Mercedes (WDD 212)

UncleBen

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2014
Posts
9,673
Reaction score
12,265
Wakuu heshima yenu, kuna garage nilipeleka gari kutengeneza

Battery ikawa down kuna mwehu mmoja akaja ku boost gari kwa kutumia terminal za battery badala ya ile external knob iliyowekwa kwa ajili ya ku boost gari

Matokeo yake dashboard haionyeshi kitu chochote ila ukiwasha gari inawaka.

imeingizwa kwenye diagnosis machine ilaleta error ya Cluster malfunction, wamefungua cluster wanaona hamna shida, fuse box pia kuangalia fuse namba 5, 18,na 28 zote zinahusika na cluster fuse ni nzima.

Wasiwasi wangu ni kununua cluster nyingine halafu ukute shida sio hiyo cluster.

Kuna yeyote ashakutana na changomoto hii msaada tafadhali.
 
Pole sana Mkuu. Samahani, garage uliyopeleka Wana deal na gari aina zote au wanamagari Yao mfano mjapani tu au ulaya pekee? Mara nyingi hizi gari ni vizuri kuwapelekea watu wanaoshughulika nazo kipekee, hapa namaanisha wale wanaojipambanua kujikita kwenye Benz, BMW, VW, Volvo n.k.

Sina uhakika na tatizo hasa itakua ni kitu Gani ila mafundi wa umeme wa magari wanawezakutoa mwanga au utatuzi wa Hilo jambo.
 
Mkuu garage niliyopeleka ni ya hao wanaosema wanatengeneza European Cars, huyo aliyeboost ni fundi rangi aliombwa sijui alisogeze hakujua njia sahihi ya boost hizi gari matokeo yake ndio ikawa hivyo,
 
Mkuu garage niliyopeleka ni ya hao wanaosema wanatengeneza European Cars, huyo aliyeboost ni fundi rangi aliombwa sijui alisogeze hakujua njia sahihi ya boost hizi gari matokeo yake ndio ikawa hivyo,

Dah! Pole kiongozi.
Hapo inafaa upate maoni ya mafundi kama wawili hivi kabla ya kufanya chochote, unaweza kujikuta unanunua vitu visivyohitajika au gari ikazidi kuharibuka vifaa vingine.

Kuna jamaa wapo Magomeni mikumi kama sikosei, wao ni umeme na kutengeneza hizi keyless za magari, na wanabadili kutoka mfumo wa funguo kuwa push to start. Amour auto kama sikosei.

Usipopata ufumbuzi unawezawashirikisha pia. Ntatafuta namba Yao nikutumie.

Mafundi nilipeleka gari ifanyiwe service ya kawaida, ilipigwa shot mfumo wa kuwashia gari ikajilick uskani na haiwaki, walivyoendelea kuhangaika nayo, niliishia kuweka engine nyingine na Bado mambo hayakua mambo, hapo ndio niliwafaham hao jamaa ilibidi wabadili mfumo mzima gari ikawa push to start.
 
Asante sana, Mkuu the Monk, hata hivyo nimeshirikisha mafundi tofauti wa haya magari na kila mmoja ana lake, kuna hawa wanao program hizi funguo na kazi zote za programing kwa ujumla, wao wanasema wakati wa ku jump start, voltage zilipanda na kushuka hivyo zika erase data zote kwenye ile chip ya data ndani ya cluster, hivyo ni kununua chip zingine halafu wa program upya data za hii Mercedes na dashboard itarudi kama kawaida

Pole kwa yaliyokukuta kaka ndio mafundi wetu hao
 

Nilishapoa ndugu yangu. Kidogo hao wa kufanya programming funguo maelezo Yao yanaeleweka.
Ukizingatia gari inawaka.

Kila la kheri na nikutakie ufanikiwe bila kuingia gharama zaidi Mkuu.
 
Nilishapoa ndugu yangu. Kidogo hao wa kufanya programming funguo maelezo Yao yanaeleweka.
Ukizingatia gari inawaka.

Kila la kheri na nikutakie ufanikiwe bila kuingia gharama zaidi Mkuu.
Asante sana mkuu, mimi kidogo nimewalewa hawa wanaosema kuna possibility ya data kuwa erased, Anyway ngoja niendelee kujipa muda na kupata maoni tofauti kabla sijaagiza chochote
 
Kiongozi hebu nenda hapo kwa dealer wa Mercedes pale pugu road wakupe ushauri stahiki. ukiwa na European car usipende kuwaamini haraka hawa mafundi wetu wa chini ya mwembe.

cheap is expensive….
 
Kiongozi hebu nenda hapo kwa dealer wa Mercedes pale pugu road wakupe ushauri stahiki. ukiwa na European car usipende kuwaamini haraka hawa mafundi wetu wa chini ya mwembe.

cheap is expensive….
Sawa mkuu, Nitaenda hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…