Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Meridian BIAO Bank .... ikiwa pale mkabala askari monument .... sasa hivi ni Tanzania Postal Bank (TPS Bank) ... zamani ilikuwa Tanzania Watch Assembly
kilichojiri ni kwamba Rais wa zamani wa zambia Keneth Kaunda alikuwa na majority shares akaziondoa ndipo bank ile ikaishia kapuni
Merdidian Biao Bank ilikuwa pale Sukari House, na ilipofilisika wafanyakazi wake wengi walichukuliwa na Stanbic Bank
Merdidian Biao Bank ilikuwa pale Sukari House, na ilipofilisika wafanyakazi wake wengi walichukuliwa na Stanbic Bank
Mkuu nadhani unachanganya na GreenLand Bank!
Hii benki kwenye mid 90s ilikuja kwa kasi sana. Baada ya muda si mrefu tukaanza kusikia imeanza kusambaratika.
Hatima yake sijui iliishia vipi. Nani anaikumbuka hii benki? Au wengi wenu humu bado mlikuwa shule za vidudu na msingi?
Aha! Nadhani wanigeria ndo hapo walipo pata hela kuanzisha na kufadhili bokoharam, si hawa jamaa kila walipo wanajiendesha kwa hela chafu!! Mfano alshaabab Somalia (uhalamia baharini) bokoharam nigeria (udanganyifu wa kitapeli) Taliban afighanistan na Pakistan ( madawa ya kulevya) heziballah Lebanon (madawa ya kulevya + money laundering ) alqaida duniani kote (money laundering ) pamoja na misaada ya kisisiri kutoka uarabuni na persia.Nyani Ngabu
Nakumbuka lile tangazo lao kwenye redio: "Meridian Biao Pan African Bank".
Hii benki ilikuwa tawi la bank ya kinigeria (West Africa). kilichofanyika ni utapeli ambao ulichangiwa na ushamba na uzembe wa BoT.
Meridien BIAO walisafirisha dola milion 30 toka Tanzania kwa kisngizio cha kwenda kusaidia matawi yake ya nje, then wakabaki na pesa ndogo sana Tanzania. BoT hawakupaswa kuruhusu ile transfer,huo ulikuwa uzembe on the side of BoT, lakini by then BoT walikuwa wana ushamba wa kudeal na private banks from abroad kwa sababu Meridien BIAO ndiyo ilikuwa bank binafsi ya kwanza ya kigeni.Hata hivyo, rushwa has to be ruled out!
Kabla ya kucollapse Tanzania, benki hii pia ilipata matatizo hayohayo Kenya na Zambia. Kuna uwezekana hawa watu walikuwa wanatumia mwanya wa ushamba wa nchi hizi kufanya utapeli.
Hii Benki haikufikisika, Bali ilifukuzwa nchini.
Iliyofilisika ni ya Uganda.
Nakumbuka hii ya hapa walikataa katukatu kua wamefilisika, walidai kua wao hawahusiani na wa Uganda but haikusaidia.
Mwishowe wakawaita wateja wao na kuwaambia chukueni tu hela zenu, lakini hatujafilisika.
Mwishowe watu wakaanza kusema kuna sababu za kidini (sizijui)