LGE2024 Meru: CHADEMA Wadai kupata ushindi katika kijiji cha Nshupu

LGE2024 Meru: CHADEMA Wadai kupata ushindi katika kijiji cha Nshupu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Kata ya Nkoaranga Kijiji cha Nshupu tumeshinda kitongoji kimoja tayari na wakala wa ccm amekimbia na kura zilizopigwa tayari tumeamishia nguvu na jeshi la Polisi wamekuja na tayari matokeo yamebandikwa.

1732721670920.jpeg

1732722890453.png
 
Kata ya Nkoaranga Kijiji cha Nshupu tumeshinda kitongoji kimoja tayari na wakala wa ccm amekimbia na kura zilizopigwa tayari tumeamishia nguvu na jeshi la Polisi wamekuja na tayari matokeo yamebandikwa.
Mmetimiza wajibu wenu wa kirai japo kwa mbinde sana.

Mnastahili pongezi
 
Wamepataje ushindi na wanasusa?
 
Chadema wanashinda kwa kura nyingi sana,hii inamaanisha kwamba hiki chama kina nguvu sana,ila utaratibu wa chaguzi zetu ndiyo unakiangusha Chadema.
 
Chadema wanashinda kwa kura nyingi sana,hii inamaanisha kwamba hiki chama kina nguvu sana,ila utaratibu wa chaguzi zetu ndiyo unakiangusha Chadema.
Utaratibu ni kamba moja nyepesi sana......muda si mrefu utakatika.
 
Huu uchaguzi ukiwa huru na haki, hakyanani ccm na chadema watagawana maeneo mengi mnoo.
 
Tunapofunga vituo vya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Taifa limeendelea kushuhudia tena ubaradhuli wa wazi na wa aibu toka kwa mamlaka zote za Serikali kushirikiana kuipatia CCM na wagombea wake ushindi wa aibu hata kwa gharama za maisha ya Watanzania.

Tunalaani mauaji na kujeruhiwa kwa wagombea, viongozi na wanachama wetu mbalimbali wakiwemo:

1) Steven Chalamila wa Jimbo la Tunduma aliyevamiwa na kukatwakatwa mapanga kikatili hadi umauti kumkuta.
2) Modestus Timbisimilwa, Mgombea nafasi ya Ujumbe wa Serikali ya Mtaa wa Ulongoni A, Kata ya Gongolamboto, Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam aliyeuwawa na askari kwa kupigwa risasi wakati wa purukushani za kuzuia kura bandia na batili kuingizwa kituo cha kupiga kura.
3)George Juma Mohammed wa Kitongoji cha Stand Kata ya Mkwese Jimbo la Manyoni Mkoani Singida aliyevamiwa nyumbani kwake na watu waliofahamika kuwa askari na kumpiga risasi iliyomsababishia umauti.

Aidha, tuna taarifa kadhaa za kujeruhiwa na kukamatwa na Polisi viongozi, wagombea, wanachama na wapenzi wetu maeneo mbalimbali ya nchi walipokuwa wakijitahidi kukamata na kuzuia kuingizwa vituoni kura bandia na batili zilizopigwa tayari kuwabeba wagombea wa CCM.

Tunataka watu wetu hawa waachiwe haraka na bila masharti yeyote.

Tunaendelea kuwasiliana na Chama kitatoa tamko rasmi zoezi hili likikamilika.

Tunaamini kinachofanyika kina maagizo na baraka zote za @SuluhuSamia na Serikali yake na au nchi iko kwenye "autopilot" na yeyote katika eneo lake ana mamlaka ya kunajisi uchaguzi anavyotaka kwani tayari wamepewa kinga na Kanuni ya 49 ya Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Ngazi ya Vijiji, Vitongoji na Mitaa inayosema, nanukuu:

"Msimamizi wa Uchaguzi, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Msimamizi wa Kituo, Wajumbe wa Kamati ya Rufani au mtumishi yeyote wa Umma aliyehusika na usimamizi wa uchaguzi hatowajibika kwa Jinai au Madai au kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu au za kiutawala kwa jambo lolote alilolifanya au kuacha kulifanya kwa nia njema wakati wa kutekeleza majukumu yake chini ya Kanuni hizi". Mwisho wa kunukuu.

Hakika Taifa lina Msiba mwingine!!
 
Chadema ni chama cha wananchi,vijana na wanyonge.
Huwezi kuwa chadema ukawa DC,au RC
 
Back
Top Bottom