Natamani ungekuwepo muda huu,sasa hivi ninapokuangalia machoni naona njia yaulimwengu ninayotaka niwepo
walisema mapenzi haya hutokea mara moja lakini sikuamini mpaka muda nilipoona nimekupenda mwifwa wangu!
Kama nimepata raha maishani mwangu ni kitu kimoja ningetaka kukibadilisha, ningekuwa nimekutana nawe tangu zamani.Mara zote unajua kunifanya nitabasamu hubby wangu hata wakati nimehuzunika.
Hakuna mwanaume duniani anayeweza kunielewa vizuri kama unavyonielewa wewe kipenzi changu,changuo langu mimi namwanaume pekee wamaisha yangu,nahisi kukukumbatia kila wakati ninapoongea nawe,najisikia salama na amani ninapokuwa karibu yako.Nafurahia mapenzi yako zaidi kuliko mtu yoyote humu duniani,siwezi kufikiria maisha yangu bila wewe yatakuwaje,marafiki zangu wananionea gere kuwa na mwanaume kama wewe unayejua nini thamani ya mwanamke!
Sifahamu umeniwekaje moyoni mwako lakini ninafurahi umenifanya hivyo na matendo yangu pekee yanaweza kuonyesha nijinsi gani ninavyokupenda hubby wangu@mwifwa!nitakupenda leo na hata kesho Ahera