Messi aifungia Barcelona bao la 500

Messi aifungia Barcelona bao la 500

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Klabu ya Barcelona inasheherekea tukio jingine la kihistoria baada ya mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi kuifungia klabu yake bao lake la 500 siku ya Jumapili.

Messi mwenye umri wa miaka 29 aliifungia Barcelona bao la kwanza katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Sevilla.

Messi sasa ameifungia Barca mabao 500 katika mechi 592,ikiwemo mechi za kirafiki huku mechi 469 zikiwa rasmi.

Messi sasa amemshinda aliyekuwa na mabao mengi Paulino Alcantara ambaye aliichezea Barcelona katika vipindi viwili vya kati ya 1912 na 1927.

Mnamo mwezi Aprili,mshambuliaji huyo alifunga bao la 500,ikiwemo mechi za kimataifa,wakati Barcelona iliposhindwa 2-1 na Valencia.

Chanzo: BBC
 
Kuna Boya Flani alikuja Na Takwimu Zake Fake Hapa Akampamba Mesi Eti Anamagoli 900+ bado Less than 100 atimize 1000...
Kwamaana hiyo Ikiwa Barcelona Klabu Pekee Aliyoichezea na Hajawahi Kuchezea Klabu Nyengine Yeyote Kaifungia Magoli 500! Je Timu ya Taifa Kaifungia Magoli 400+???
Wacheni Kumpa Messi Sifa Za Kijinga...
Messi ukimchanganyia Na Ya Timu ya Taifa Hatimizi Hata Magoli 600...


Atakaeuona Hule Uzi Uliompaisha Messi Kwa Magoli Fake Naomba Aulete hapa
 
La Pulga nimeona jana walivyomchezea rafu mpaka kiatu kikamvuka akaaza kukivaa uwanjani refa akampiga kadi ya njano Andunje akaamua kwenda nje kuvaa kiatu ila alipatwa na hasira sana pia mechi ya jana ilikuwa ngumu sana kwa Barca
 
Back
Top Bottom