Messi aongoza mauaji ya Paraguay

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Akipiga pasi tatu za goli na kuanzisha mashambulizi mengine matatu,Lionel Messi ameiongoza Argentina kuisambaratisha Paraguay 6-1 katika nusu fainali ya Copa America. Messi,akicheza kama kiungo mshambuliaji katika kikosi cha Tata Martino,alikuwa kwenye kiwango bora alfajiri ya leo.

Mabao ya Argentina yamefungwa na Angel Di Maria aliyefunga mawili na moja moja toka kwa Javier Pastore,Marcos Royo,Aguero na Higuain.

Messi sasa kama Nahodha ameiongoza Argentina kucheza fainali ya pili mfululizo baada ya ile ya Kombe la Dunia ambapo Argentina ilifungwa bao moja kwa bila na Ujerumani. Fainali ya Copa America itachezwa Jumamosi baina ya wenyeji Chile na Argentina. Mara ya mwisho Argentina kutwaa ubingwa ilikuwa ni 1993.
 

Huyu andunje Lazima awe mchezaji bora wa dunia kwa mara ya 5. Rekodi ambayo sidhani kama itavunjwa kirahisi.
 

Na Kuna Mchezaji Mmoja Hapo Zacharria Hanspoppe Anamfuta Leo Ili Kuja Kuichezea Simba Sports Club. Simba Ya Msimu Ujao Itakuwa Kama Argentina Vile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…