Messi arejea timu ya taifa ya Argentina na kuipa ushindi

Messi arejea timu ya taifa ya Argentina na kuipa ushindi

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Mchezaji bora wa kandanda ulimwenguni,Lionel Messi,alfajiri ya leo alirejea kwenye kikosi cha timu yake ya taifa ya Argentina na kukipa ushindi dhidi ya Uruguay.

Bao lake la uwezo binafsi la dakika ya 42 lilitosha kuwapa ushindi Argentina na kuwaweka kileleni kwenye msimamo wa kufuzu kombe la dunia kwa bara la Amerika ya Kusini kwenye timu kumi. Argentina sasa ina alama 14,alama moja zaidi ya Uruguay na Colombia wenye alama 13 katika michezo 7.

Katika michezo mingine,Brazil iliichapa Ecuador bakora 3-0 huku Mabingwa wa bara hilo Chile wakizabwa mabao 2-1 na Paraguay. Katika msimamo,Brazil iko nafasi ya tano ikiwa na alama 12.
 
Mchezaji bora wa kandanda ulimwenguni ni Messi au Christiano Ronaldo?
 
Mchezaji bora wa kandanda ulimwenguni ni Messi au Christiano Ronaldo?
NI LEO MESSI
1472794216108.jpg
1472794222299.jpg
1472794231766.jpg
1472794238825.jpg
1472794246047.jpg
NA SI CRISTINA MMOROCO
1472794276577.jpg
 
Huyo ndiye mfalme wa soka, thank you so much Petro Mselewa kwa taarifa
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Mfalme wa soka yuko mmoja tu pelleee wa brazili baasi

Haya mkuu sio mbaya kujifurahisha,nisikufanye ukakosa usingizi buree.. najua unaumia sana wanapotajwa the Kings Messi and Diego Maradona,, huyo mr offside wako anajua fiika kazidiwa mbali sana na These guys from the same country "Argentain"
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Back
Top Bottom