Mchezaji bora wa kandanda ulimwenguni,Lionel Messi,alfajiri ya leo alirejea kwenye kikosi cha timu yake ya taifa ya Argentina na kukipa ushindi dhidi ya Uruguay.
Bao lake la uwezo binafsi la dakika ya 42 lilitosha kuwapa ushindi Argentina na kuwaweka kileleni kwenye msimamo wa kufuzu kombe la dunia kwa bara la Amerika ya Kusini kwenye timu kumi. Argentina sasa ina alama 14,alama moja zaidi ya Uruguay na Colombia wenye alama 13 katika michezo 7.
Katika michezo mingine,Brazil iliichapa Ecuador bakora 3-0 huku Mabingwa wa bara hilo Chile wakizabwa mabao 2-1 na Paraguay. Katika msimamo,Brazil iko nafasi ya tano ikiwa na alama 12.