Messi asimamishwa na PSG kwa wiki mbili bila Mshahara

Messi asimamishwa na PSG kwa wiki mbili bila Mshahara

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Klabu ya Paris Saint-Germain imeripotiwa kumsimamisha mshambuliaji Lionel Messi kwa wiki mbili bila mshahara baada ya Nyota huyo raia ya Argentina kukwepa mazoezi ya klabu hiyo na kukwea pipa kuelekea Saudi Arabia bila idhini ya klabu.

Upande wa Messi bado haujatoa ufafanuzi juu ya sakata hilo na unasubiri tamko rasmi la miamba hiyo ya Ufaransa.

Messi hataweza kucheza kwa wiki mbili zijazo ikiwa hakutakuwa na mabadiliko kwenye adhabu hiyo iliyoamuliwa na PSG.
 
Kweli ,hajafanya starehe miaka mingi Sana ,kikubwa asijisahau
 
PSG wapate manager.. waachane na kina messi na neymar.. wajenge timu yao kumzunguka Mbappé.
 
Au Man city wampe pesa Messi ili aziingize kwenye Akaunti ya PSG ili avunje mkataba kama alivyofanya Feisal.
 
Back
Top Bottom