poposindege
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 453
- 175
[h=2]Hat-rick ya Messi dhidi ya Rayo Vallecano ilivunja rekodi ya mmoja wa wanasoka bora duniani, Pele iliyokaa kwa zaidi ya miaka 50.[/h]Mabao hayo yamemfanya Messi kuipita rekodi ya ufungaji mabao ya Pele katika misimu yake sita ya mwanzo katika soka. Kuanzia msimu wa 2009/10, Messi ametimiza mabao 315 kutokana na Hat Trick yake ya wikiendi iliyopita.
Kwa upande wa Pele, rekodi hii aliishikilia kwa zaidi ya miaka 50 baada ya kufunga mabao 313 kuanzia mwaka 1958 mpaka 1963 na tangu hapo hakuna mwanasoka ambaye aliwahi kufunga mabao mengi katika kipindi kifupi.
Hata hivyo nyota huyo wa Barcelona anatarajiwa kufanya maajabu zaidi msimu huu kwani amebakiwa na mechi 19 mpaka msimu uishe hivyo kuwa na fursa ya kufunga magoli mengi zaidi.
Hii ni rekodi nyingine ya Pele ambayo Messi anaivun ja baada ya kuvunja ile ya kuwa na magoli mengi ndani ya mwaka mmoja iliyowekwa na Pele mwaka 1958 na kuvunjwa na Messi mwaka 2012.
Aidha mwaka huohuo 2012, Messi alivunja rekodi ya Mjerumani Gerd Muller ya kufunga mabao zaidi ya 85 ndani ya mwaka mmoja.