SI KWELI Messi na Ronaldo wamekutana na kucheza pamoja kama video hii

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1

Your browser is not able to display this video.


​
 
Tunachokijua
Uchambuzi wa video kupitia nyenzo za kubaini maudhui yaliyotengenezwa kwa Akili Unde unabainisha kuwa sauti na picha zote zina alama za kidijitali (digital watermarks) ambazo hutumiwa na Google kutambua maudhui yaliyotengenezwa au kubadilishwa kwa kutumia AI.

Kadhalika zipo hitilafu au mapungufu ya kimuonekano ambapo ukiangalia kwa makini mandhari ya nyuma na nyuso za watu waliopo, utaona “glitches” na mienendo isiyo ya kawaida ambayo ni ya kawaida katika video za AI. Kwa mfano, kamera inaposogea, uwiano wa wachezaji na watu wanaowazunguka hubadilika kidogo kwa namna ambayo haiwezi kutokea katika hali halisi.

Hata hivyo hakuna kumbukumbu yoyote inayoonesha kuwa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo waliwahi kukutana katika mazingira kama haya. Kutokana na hadhi yao, tukio kama hili lingekuwa habari kubwa duniani na kuripotiwa na vyombo vikuu vya michezo ambapo kupitia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) imebainika kuwa hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichoripoti kuhusu tukio hilo.

Video hii inayoonekana kuwa halisi sana inaendelea kuwa ya kawaida kama njia ya kuunda matukio ya kubuni kwa ajili ya burudani, lakini katika kesi hii, mkutano wa kihistoria kati ya mastaa hawa wawili haujawahi kutokea katika uwanja huu.​
Kuna AI videos nying sana nazionaga Messi na Eonaldo wakiwa pamoja wanazurura mitaani nchi mbalimbali,zile video mtu ukiambiwa ni AI unakataa maana hazina kasoro hata asilimia 10 tu hata hii ni mojawapo
 
Sasa mkuu hii apo wanavyoruka....si unajua tu AI
 
Hili ni tukio la kutengeneza mastaa hawa hawajawahi kukutana popote na kufanya jambo kama hilo
 
Hili ni tukio la kutengeneza mastaa hawa hawajawahi kukutana popote na kufanya jambo kama hilo
Ndiyo, video inaonekana kuwa halisi lakini ukweli ni hakuna tukio kama hilo la hawa jamaa, halijaripotiwa na vyanzo vya kuaminika.
 
Kuna Moja Tangazo limetoka Leo la LEGO toys kampuni ya huko Denmark wapo wanne Mbappe, Vinius Jr sijui ndo hivyo pamoja na hao Cr na Messi wapo mezani Ile ni ukweli
 
Hii ai miaka ya mbele wanaume kukamatwa unachepuka ni mpaka iwe red handed, hivi vingine tutasingizia ni ai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…