Messi: Sifikirii kucheza Kombe la Dunia 2026

Messi: Sifikirii kucheza Kombe la Dunia 2026

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
LIONEL Messi amethibitisha kuwa “hafikirii” kama atacheza Kombe lingine la Dunia baada ya kuiongoza Argentina kutwaa ubingwa wa mashindano hayo mwaka jana nchini Qatar.

Messi ambaye ana umri wa miaka 35 alisema hayo katika mahojiano na vyombo vya habari vya China kuhusu mustakabali wake kwenye michuano hiyo mikubwa ambayo inayofuata itafanyika mwaka 2026 kwa ushirikiano wa nchi tatu, Marekani, Canada na Mexico.

“Nimesema mara kadhaa hapo awali kwamba sifikirii hivyo, kwamba hiyo (2022) lilikuwa Kombe langu la mwisho la Dunia,” alisema alipoulizwa na Titan Sports ya China kwenye mahojiano.

“Nitaona jinsi mambo yanavyokwenda, lakini kwa nadharia sidhani kama nitakuwepo kwa Kombe lijalo la Dunia,” aliongeza.
 
Hana baya GOAT
amemaliza kalibu Kila kitu kwenye mpira
 
Back
Top Bottom