Nakumbuka wakati wa Euro 2000, kulikuwa na maswali na malumbano mengi sana kati ya wadau wa soka waliokuwa wanajiuliza Zinedine Zidane na Louis Figo ni nani mkali zaidi. Hawa wachezaji enzi hizo walikuwa katika kiwango cha juu mno. Niliwafanyia wadau uchambuzi yakinifu kuwaelezea hawa wafalme wawili wa enzi hizo na kuonekana dhahiri kuwa nani alikuwa zaidi.
Moja ya kitu ninachokumbuka, vyombo mbalimbali vya kimataifa baada ya ile michuano walikuwa wanacomment kuwa Louis Figo ni mchezaji bora kabisa katika Euro 2000, ILA UKIMUWEKA ZIDANE PEMBENI. Maana yake ilikuwa ni kwamba, wakati Figo ndio alikuwa The world best footballer, Zidane alikuwa katika level nyingine baada ya ubest, sasa kwa kiingereza hakuna neno linalomchambua mtu aliye zaid ya best. Maana kuna good, better na best. Labda extremely best !!! Ilikuwa kila Zizzou alipokuwa anacheza, commentators walikuwa wanatafuta maneno ya kumfit km, wonderful, classic, excellent, extraordinaly na mengineyo ya mfano huu…
Sasa, nirudi kwenye mada kuu. Wakati dunia nzima saizi ya wapenzi wa kandanda aka soka ikiwa inajiuliza ni nani mkali kati ya Crhistiano Ronaldo na Leonel Messi, mimi nikiwa kama mchambuzi niliyebobea katika soka la kimataifa nakuletea kwa kina uwezo wa hawa mastar wawili wanaoishika dunia ya soka kwa sasa.
Nitafanya outlining ili nieleweke vizuri. Hapa nitaweka point kumi na mbili muhimu za kuwalinganisha halafu mwisho nitaconclude. Nikianza na Christiano Ronaldo,
CR ana sifa zifuatazo,
- Physical appearance (urefu 1.86m au 6.1ft) inampa advantage kama mchezaji katika position yoyote.
- Anaweza kutumia miguu yote miwili vizuri kabisa, hii inamfanya amudu kucheza nafasi nyingi bila tabu yoyote.
- Ana uwezo mkubwa wa kutumia kichwa. Hii inamfanya aweze vizuri kufunga magoli ya kichwa hapa pointi ya kwanza (urefu) pia inamwongezea hii advantage.
- Ana uwezo mkubwa wa kupiga faulo. Ikiwa ni pamoja na kuwa ni mpiga penati mzuri achilia mbali penati kadhaa muhimu ambazo ashawahi kukosa.
- Ana uwezo mkubwa wa kuipasua ngome ya wapinzani, hii nikiwa namaanisha ni mwepesi wa kupiga chenga na pia ana spidi kali inayomfanya awe tishio kubwa kwa wapinzani
- Anauwezo mkubwa sana wa kufunga magoli akitokea upande wowote wa uwanja na kwa mguu wowote. So far ashafunga goli 22 za Laliga katika mechi 19, msimu uliopita alifunga magoli 26 katika Laliga pia 4 za champ ligi. Mpaka sasa Ronaldo ashafunga magoli 65 katika mechi 64 akiwa Madrid.
- Ana uwezo wa kucheza kama kiungo wa pembeni, pia anauwezo mkubwa wa kucheza km mshambuliaji wa kati. Pia CR anaweza akacheza nyuma ya mshambuliaji wa mwisho. Hii inamfanya awe flexible sana na formation nyingi za kiuchezaji.
- Ni mzuri sana wa kupiga pasi za mwisho. Kwenye statistics so far kwenye Laliga ametoa pasi 6 na pia kwenye UCL ametoa pasi 2.
- Ni mwepesi wa kuflustrate timu yake inapokuwa down, hii inamfanya asiweze kuwika katika mechi ngumu. Hii inamfanya awe amefunga mara chache sana anapocheza mechi ngumu.
- Hajaonyesha kiwango chochote cha ajabu akiwa na timu yake ya taifa.
- Pamoja na kuwa anatumia miguu yote, CR si mzuri sana akiwa anashambulia akitokea kushoto.
- Hana uwezo kabisa wa kusaidia defence ya timu yake.
Nikija kwa Leonel Messi.
Kwa kufuatilia hizo pointi 12, naamini utakuwa umeweza kupata picha halisi ya hawa wanasoka wawili wanaowika sasa katika medani ya soka. Katika maeneo mengi uwezo wao unaelekeana, na kama ni kuzidiana ni katika kiwango kidogo.
- Physical appearance yake (urefu 1.69m au 5.58 ft) haimpi advantage kubwa ya kucheza namba nyingi uwanjani na ndio maana alivyoanza soka na Barca alitumika zaidi kama winga wa kulia.
- Anauwezo mkubwa sana wa kutumia mguu wa kushoto, ni mwepesi sana, hii inamfanya kutoonekana udhaifu wake wa kuwa na uwezo mdogo sana wa kutumia mguu wa kulia.
- Uwezo wake wa kutumia kichwa ni mdogo kwa sababu ya kimo chake, ila kutokana na wepesi wake mara chache amekuwa akifunga magoli makali sana kwa kichwa, km goli la 2 na Man U fainali ya UCL 2009 aliweza kuruka juu na kuwaacha magiant Vidic na Ferdinand na pia alishafunga goli kwa kuruka juu na kuusindikiza mpira kwa mkono katika mechi na Espanyol, ni goli sawa kabisa na alilofunga Maradona maarufu kama mkono wa mungu.
- Si mpigaji wa mara kwa mara wa faulo, ila mara kadhaa amekuwa akifunga kwa faulo. Pia si mpigaji wa penati, imetokea mara chache sana kwa Messi kupiga penati.
- Ni extremely dangerous anapokuwa na mpira, anauwezo mkubwa sana wa kupiga chenga, ni mwepesi sana na pia anapokuwa na mpira ni vigumu sana kwa mabeki kujua anachotaka kukifanya, kama kutoa pasi, kupiga shuti au kupiga chenga. Hii inafanya awe hatari mno hata anapobaki na mabeki hata kama ni wawili au watatu.
- Ana uwezo mkubwa sana wa kufunga akitokea upande wowote wa uwanja, ila kwa kutumia mguu wa kushoto. Ana goli 18 za Laliga katika mechi 19, msimu ulioisha alifunga magoli 34 katika mechi 34 za LaLiga, alifunga magoli 48 katika michuano yote na Barca na pia ameshafunga magoli 6 ya UCL ktk mechi 6 msimu huu.
- Japokuwa Messi anatumia sana mguu wa kushoto, ila anauwezo wa kucheza namba zote za mbele. Anauwezo wa kucheza kama kiungo wa pembeni, ni hatari sana anapokuwa anashambulia tokea kulia, pia anauwezo wa kucheza nyuma ya mshambuliaji, mshambuliaji wa mwisho au kama attacking midfielder. Ni hatari sana anapokuwa anacheza kama kiungo wa kushambulia, nyuma ya mchambuliaji mmoja au wawili.
- Ni mpiga pasi za mwisho bora kabisa katika ulimwengu wa sasa. So far ana pasi za mwisho 13 katika Laliga.
- Messi yupo humble, ni mchezaji aliyetulia asiye na makeke, na hata timu yake inapozidiwa si rahisi kumuona ameflustrate.
- Messi pia bado hajaonyesha uwezo mkubwa kwenye timu ya taifa.
- Japokuwa hatumii kabisa mguu wa kulia, Messi ni hatari sana anaposhambulia kutokea kulia. Hii imefanya udhaifu wake wa kutotumia mguu wa kulia usionekane.
- Si mzuri kabisa kwenye kusaidia defence.
Pamoja na hayo, Messi ni bora zaidi kwa sababu anaskills ya hali ya juu sana ukilinganisha Ronaldo. Kwakiwango kikubwa, Ronaldo kasi yake ndiyo humfanya awe hatari anapokuwa na mpira, lakini Messi skills yake ndiyo inayomfanya awe hatari sana, maana anapokuwa na mpira huwezi jua anataka kufanya nini, na ndio maana ukiangalia katika upigaji wa pasi za mwisho Messi anatisha mno. Kuna vigezo vingine vingi tu vinavyowahusu, ila kwa kuwa maelezo yanakuwa marefu nimeamua kuishia hapo maana hili si gazeti.
msimu ulopita nani aliongoza ?messi yuko vizuri mno japo ronaldo nae yuko vizuri bt nampa messi 60% ya kuwa mfungaji bora dhidi ya ronaldo kwa msimu huu