Metacha Mnata asimamishwa kazi na klabu ya Yanga

Metacha Mnata asimamishwa kazi na klabu ya Yanga

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
yangapic

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umemsimamisha kipa wake, Metacha Mnata kutokana na utovu wa nidhamu alioufanya kwa mashabiki baada ya mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa jana usiku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Klabu hiyo imesema kuwa, uongozi umesikitishwa na kitendo kisichokuwa cha kiungwana alichokifanya Metacha hiyo anasimamishwa hadi hapo suala lake litakapofikishwa mbele ya kamati ya nidhamu ya klabu hiyo.

Pia, Uongozi umeomba radhi wanachama, wapenzi, mashabiki na wadau wa michezo kwa kitendo hicho alichokifanya Mnata

Jana usiku baada ya mchezo wa Yanga dhidi ya Ruvu Shooting kumalizika kipa huyo wa Wanajangwani, Metacha Mnata alionyesha ishara mbaya kwa kuwanyoshea vidole mashabiki waliokuwa wakimzomea.

Hiyo ni baada ya Metacha kuzozana na baadhi ya wachezaji wenzake na alipokuwa anaenda vyumbani ndio aliwaonyeshea ishara hiyo kwa mashabiki wa Yanga.

Mashabiki hao ambao hawakufurahishwa na kitendo hicho waliamua kulizunguka gari la timu yao wakimshinikiza kumtaka Metacha aliyetibua furaha yao ya kuifunga Ruvu Shooting

''Tunamsubili aje atuambie kwanini anatuonyeshea vidole kama tusipompata hapa tutamfata nyumbani kwake (akitaja anapoishi mchezaji huyo),” alisikika mmoja wa mshabiki hao.
 
Kipa ana stress...mashabiki nao wana stress...tabu tupu
 
Lakini alifanya kitendo kisicho cha ki-uana michezo japo nimeona ameomba radhi kupitia mtandaoni. Wachezaji wetu hawako makini kwenye maswala ya kinidhamu, wana mambo ya kihuni-huni sana.
 
Hivi Yanga ina watu wa aina gani? Na wanaumbwa wapi? Hakuna utulivu kabisa kwa hawa jamaa.
 
Back
Top Bottom