Methali na misemo inayoelezea hali ilivyo sasa nchini

Methali na misemo inayoelezea hali ilivyo sasa nchini

Companero

Platinum Member
Joined
Jul 12, 2008
Posts
5,606
Reaction score
1,711
1. Samaki mmoja akioza wote wameoza
2. Usipoziba ufa utajenga ukuta
3. Siku za mwizi ni arobaini
4. Hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho
5. Kikulacho ki nguoni mwako
6. Kipya kinyemi ingawa kidonda
7. Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi
8. Jungu kuu halikosi ukoko
9. Lisemwalo lipo kama halipo linakuja
10. Avumaye baharini papa kumbe wengine wapo
11. Dalili za mvua ni mawingu
12. Kukopa harusi kulipa matanga
13. Kozi mwana mandanda kulala na njaa kupenda
14. Mwenda tezi na omo hurejea ngamani
15. Fumbo mfumbie mjinga mwerevu huling'amua
16. Lila na fila havitangamani
17. Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza
18. Sikio la kufa halisikii dawa
19. Utavuna ulichopanda
20. Amani haipatikani ila kwa ncha ya upanga
 
kikwete ile siku anatangazwa na ccm kuwa mgombea wa urais
back in 2005
nilijikuta nasema

be carefull on what you wish for,because you might get it...
 
Back
Top Bottom