Methali. . . .

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,009
Reaction score
60,629
Embu tujaribu kuzi'mordenize' kidogo ziendane na maisha ya kileo.

. . . Lisemwalo lipo kama halipo . . . HALIPO.
. . . Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu, lakini hakosi KUJINASUA.
. . . Pole pole YACHELEWESHA.
. . . Dawa ya moto ni MAJI.
. . . Fuata nyuki UTOLEWE MANUNDU.
. . . Kawia UCHELEWE.
. . . Mgeni njoo MWENYEJI AINGIE GHARAMA.
. . . Samaki mmoja akioza MTUPE.
. . . Ukitaka uzuri SHARTI ULIPIE.
 

. . . Aliyejuu MFATE HUKO HUKO
. . . Asiyekujua USIMJUE
. . . Asiyesikia la mkuu HUSIKILIZA LA MDOGO
. . . Maisha yakikupa mgongo YASHIKE MASABURI
. . . Mchagua jembe ANA AKILI
. . . Mchimba kisima HUEPUKA ADHA ZA EWURA
. . . Mtaka yote HUPATA JAPO MOJA
. . . Mtoto akililia wembe USIMPE ATAJIKATA
. . . Mwerevu hujinyoa KUBANA MATUMIZI
. . . Penye udhia KIMBIA
. . . Ukiona vyaelea VIMO SAFARINI
. . .
Kwa mifano zaidi fuatilia thread ya Bujibuji alikuja nayo ya METHALI MPYA:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-lugha/42700-methali-mpya-3.html
 

Hahahahahaha. . .ahsante MammaMia. .

. . . Aisifuye mvua KAONA MAFURIKO YA DAR.
. . . Asieona HUONYESHWA.
. . . Adhabu ya kaburi AIJUA MCHIMBAJI.
. . . Mvumilivu HULA MBOVU.
. . . Asiyekubali kushindwa NDIE MSHINDI.
. . . Atangae na jua HUUNGUA.
. . . Fadhila ya punda KUBEBA MZIGO.
. . . Ukitaka cha uvunguni SOGEZA KITANDA.

. . . .
 
nyie ndio wahenga wa siku zijazo......keep it up.
Vitukuu vyenu vitakuwa vinatumia hizi methali, vitakuwa vinasema 'wahenga walisema samaki mmoja akioza mtupe'

bila kujua hao 'wahenga' ni akina lizzy.
 
nyie ndio wahenga wa siku zijazo......keep it up.
Vitukuu vyenu vitakuwa vinatumia hizi methali, vitakuwa vinasema 'wahenga walisema samaki mmoja akioza mtupe'

bila kujua hao 'wahenga' ni akina lizzy.
Hahaha. . . asipotupwa ataozesha wenzake.

Alafu wahenga sie tunazingatia uhalisia, vitukuu lazima watukubali.
 
Mwenda kwao kawakumbuka ndugu ze
 
Mwenda kwao kawakumbuka ndugu ze

Niiiice

. . . Usisafirie nyota ya mwenzako KAMA HUJALIPIA.
. . . Adui aangukapo MKANYAGE.
. . . Ajuaye mengi KAJIFUNZA.
. . . Bahati ya mwenzio YAWEZA KUWA YAKO.
. . .
 

hahahaha.
 
> Mficha uchi,
Atakua amevaa nguo.
> Kila ndege ,
huruka Airport.
> Njia ya muongo,
Kua mwanasiasa. >Mla mlaleo,
mla kesho leo ana saumu.
> Usipo ziba ufa,
mwizi atachungulia ndani.
>Mpanda Farasi wawili,
huyo mwanasarakasi.
> Kwenye miti mingi,
hakuna wakuikata.
> Polepole siyo mwendo,
huyo hana nauli.
 
Alalaye usimwamshe; ukimwamsha, atapoteza usingizi
Aliyekando, amekupisha njia
Cha mlevi huliwa na breweries
akumulikae mchana usiku atalala

Mfuata nyuki hakosi manundu
Dawa ya moto ni maji


 
Mchuma janga..... Imekula kwake!
Mchumia juani..... yupo jangwani
Asiyekuwepo machoni...... unam-delete
 
Simba mwenda pole anamuogopa yanga

Aisifiaye mvua hajawai kuishi mabondeni
 
Mficha uchi, hajui raha ya mapenzi.

Nyani akitaka kuona kundule, atumie kioo.

Ukimshtaki fisadi, utaharibu uchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…