Shadow7
JF-Expert Member
- Sep 28, 2020
- 24,606
- 39,289
Watafiti nchini Mexico wanadai kuwa wamebuni mtindo mpya wa Barakoa (mask) ambao utamuwezesha mtumiaji kuweza kula, kunywa na hata kuzungumza huku akiwa bado amejilinda dhidi ya Virusi vya Corona.
Barakoa hiyo ambayo imezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii na kuitwa ‘maski za pua’ zilionekana kuvaliwa na mwanaume mmoja na mwanamke ambao majina yao hayakuweza kutambuliwa wakiwa wamekaa katika mgahawa wakipata chakula.
Kipande cha video ambacho kilisambaa kupitia shirika la habari la Reuters walionekana wawili hao wakivua Barakoa zilizoziba mdomo na ndani yake kukiwa na hizo ambazo si zakawaida huku wakipata chakula wakiwa pamoja.