Muuza Kangala
JF-Expert Member
- Jul 21, 2021
- 1,242
- 4,813
Mstahiki Meya wa Kinondoni, Songoro Mnyonge ametoa wito kwa jamii kuacha kutumia ngono kama kazi, akisema ni kinyume na sheria za nchi. Akiongea kwenye kipindi cha SupaBreakfast, Meya Mnyonge amesema asilimia 30 tu ya kondomu zinazowekwa kwenye maeneo ya biashara zinachukuliwa na kutumiwa na wafanyabiashara hao.
Ameongeza kuwa, hospitali ya Mwananyamala inashuhudia idadi kubwa ya vijana zaidi ya 2000 wanaotumia Methadone na baada ya kumaliza hawataki kuondoka. Hii imesababisha usumbufu kwa majirani, na Meya Mnyonge aliwataka wananchi kutumia huduma hiyo kwa uangalifu na kutoshiriki katika tabia ya kuzurura.
Meya Mnyonge amesema serikali itachukua hatua dhidi ya biashara ya ngono, akisema kwamba hawawezi kuruhusu tendo la faragha kufanyika hadharani kwa namna yoyote ile. Aliendelea kusema kwamba hata tovuti za ngono zilifungwa na hakuna yeyote aliyeathirika, na kwamba inawezekana kusitisha biashara hiyo.
Alitoa wito kwa jamii kuacha kufanya ngono katika mazingira ya ajabu na kuacha kutumia ngono kama kazi. Alisisitiza kwamba tendo la ndoa ni tendo la faragha kwa mila za Afrika na hata wazungu hawawezi kulifanya hadharani.
Meya Mnyonge amesema kwamba kufanya ngono katika mazingira ya ajabu ni kinyume na maadili ya kiafrika na kwamba kama mtu atajigeuza kuwa mnyama, atakabiliwa na sheria. Aliwataka wananchi kutii sheria na kuishi kwa kufuata maadili ya kiafrika.