Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Mambo yanazidi kuwa moto, kila mtu anajitafutia ka angle a kuonekana
kazi kwenu wananchi!
Wananchi mkoani Mtwara, wamehimizwa kujitokeza kupiga kura katika kuchagua viongozi ili kutekeleza haki yao ya msingi kuchagua na kugombea kama ni kiongozi. Hayo ameyasema Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Bi Shadida Ndile jana tarehe 02/11/2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kata ya kisungure iliyopo Mikindani.
Hata hivyo amesema kua kuelekea uchaguzi huo Shadida Ndile ameamua kuongeza hamasa na kufungua ligi ya kata na itajulikana kwa jina la Uchaguzi Ndile Cup imbalo litaanza tarehe 09/11/2024 katika viwanja vya Titanic vilivyopo Mikindani na ikiwa ni lengo la kuongeza hamasa na kukumbusha wananchi kujitokeza kupiga kura ifikapo tarehe 27/11/2024.
Mashindano hayo yatatoa mshindi wa kwanza ambae atapata kiasi cha shilingi milioni Moja (1,000,000) na mshindi wa pili atapata shilingi laki tano (500,000) kama sehemu ya zawadi katika mashindano hayo.
Safari Media
Mambo yanazidi kuwa moto, kila mtu anajitafutia ka angle a kuonekana
kazi kwenu wananchi!Wananchi mkoani Mtwara, wamehimizwa kujitokeza kupiga kura katika kuchagua viongozi ili kutekeleza haki yao ya msingi kuchagua na kugombea kama ni kiongozi. Hayo ameyasema Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Bi Shadida Ndile jana tarehe 02/11/2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kata ya kisungure iliyopo Mikindani.