Meya Mstaafu DAR: Deni la Machinga Complex halilipiki na halitalipika

Meya Mstaafu DAR: Deni la Machinga Complex halilipiki na halitalipika

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salam 2015-2019, Isaya Mwita akizungumza na Mwananchi nyumbani kwake Kigamboni Dar es Salaam alisema makubaliano ya awali kati ya NSSF na Jiji la Dar es Salaam juu ya ujenzi huo ilikuwa ni mkopo wa Sh9 bilioni na kuwa kabla ya kumaliza ujenzi gharama ilifika Sh12 bilioni.

“NSSF ilipewa idhini ya kujenga na kutukabidhi ili tuliendeshe na kuanza kulipa hilo deni la Sh12 bilioni, hadi naingia madarakani 2015 tayari deni lilikuwa limefikia Sh37 bilioni,” alisema Mwita.

Alisema, wakati huo walikaa vikao mbalimbali na NSSF kuzungumzia deni hilo na uhalali wake huku wakiomba nyaraka za ujenzi lakini hawakuwahi kuziona.

“Hakuna mtu yeyote anayeweza kupata nyaraka za lile soko, si mkaguzi wa ndani wa Serikali wala wa nje, hawezi kupata zile nyaraka,” alisema.

Kutokana na sintofahamu ya deni hilo, Mwita anashauri kusimamishwa kwa riba ambayo ni wastani wa Sh5 bilioni hadi Sh6 bilioni kwa mwaka.

Alisema katika uongozi wake walianza kulipa deni hilo lakini sasa “haliwezi kulipika na halitakaa kulipika.”
Meya wa sasa wa Jiji hilo, Omary Kumbilamoto, amelieleza Mwananchi hivi karibuni kuwa hawajaanza kulipa deni hilo na soko husika lipo chini ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

“Soko bado lipo chini ya ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kuondolewa jiji na uhakiki unafanyika huko,” alieleza.

Kauli ya Kumbilamoto inathibitishwa na Steven Sindaguru, ofisa usimamizi fedha katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiongeza kuwa ofisi hiyo inaratibu majadiliano baina ya pande hizo mbili --NSSF na Jiji la Dar es Salaam kuhusu deni hilo.

Hata hivyo, Sindaguru alieleza kuwa, taarifa za deni hilo ambazo ziliwahi kutolewa na Mwita zilikuwa sahihi, ingawa kwa sasa si sahihi kulingana na deni hilo kubadilika kila saa, siku na mwezi.

Alifafanua kuwa deni ambalo lipo kwenye majadiliano lina riba pamoja na adhabu, hivyo takwimu za sasa zinapaswa kupigwa kulingana na wakati uliopo.

Mkopo uliotolewa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa Soko la Machinga Complex umekuwa mfupa mgumu kurejeshwa na hadi sasa takwimu zake zimebaki kizungumkuti.

Wakati uongozi wa Jiji la Dar es Salam ukisema ulikabidhiwa soko hilo deni likiwa limefikia Sh12 bilioni kutoka Sh 9 bilioni zilizokuwa kwenye makubaliano ya awali, NSSF inasema fedha zilizotumika kulikopesha Jiji katika ujenzi huo kati ya mwaka 2007 na 2012 zilikuwa Sh15.9 bilioni na riba ni asilimia 14.44 kwa mwaka.

Mpaka sasa, NSSF imethibitisha kuwa Jiji la Dar es Salaam limesharejesha Sh80 milioni kwenye sehemu ya deni wanalodaiwa na majadiliano yanaendelea ya mfuko huo, Jiji na Serikali.

Mkurugenzi wa Uwekezaji NSSF Gabriel Silayo akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, alisema majadiliano yanaendelea kati ya Jiji la Dar es Salaam, Serikali na NSSF ili kuona njia bora ya kulipa deni hilo.

Hali ikiwa hivyo, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ripoti zake alisema mkopo wa awali wa soko hilo ulikuwa Sh13.5 bilioni huku riba ya mtaji ikiwa Sh2.77 bilioni ambato ingelipwa kwa miaka 11, masharti ambayo yalipingwa na halmashauri mwaka 2016.
 
Hii nchi mambo yake ni mengi sana na suluhu pekee ni mapinduzi ya raia na nchi kuwa chini ya baraza maalum hata mwaka kabla yakuhusisha watanzania woote kwente reform.
 
“Hakuna mtu yeyote anayeweza kupata nyaraka za lile soko, si mkaguzi wa ndani wa Serikali wala wa nje, hawezi kupata zile nyaraka,” alisema.

NIKI ISHA STAAFU MTAZIPATA TU, KAENI KWA KUTULIA.

Alisikika mlevi mmoja akiongea huko Costa Rica
 
Back
Top Bottom