Mbatizaji Mkuu
Member
- Jul 19, 2020
- 39
- 128
MEYA RAIBU ATAKA KAZI IENDELEE NA IKAMILIKE
Utekelezaji wa sheria na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan umefanyika katika manispaa ya Moshi kwa kutoa mikopo yenye Tshs Milioni 302,904,000 kwa vikundi 133, vikujumuisha vikundi 91 vya Wanawake, 39 vya Vijana na vitatu 3 vya walemavu.
Akiongea katika hafla ya kukabidhi mikopo hiyo ambayo ni takwa la kisheria Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Juma Raibu Juma ametoa maangalizo na tahadhari kwa wanavikundi hao Kuwa ni marufuku kuweka fedha hizo nyumbani bali miamala yote ifanyike kwa njia ya kibenki ili kudhibiti matukio ya uporaji na udanganyifu.
Pia Meya Raibu vikundi vyenye lengo la kukopesha fedha hizo wahakikishe wanakopa kwa malengo maalumu yenye tija na sio kufanyia anasa jambo linalokuja kuwawia ugumu kwenye urejeshaji wa mikopo hiyo isiyokuwa na riba.
Meya Raibu amepiga marufuku vikundi vya vikoba vya Manispaa ya Moshi kukopeshana fedha za vikundi bila maridhiano ya vikao na Sio kauli ya mwenyekiti wala katibu Kujiamulia bila kufuata Utaratibu.
"Tutachukua hatua kali kwa vikundi vitakavyoshindwa kurejesha fedha hizi ambazo zimeondolewa riba, tunataka mchukue mlipe na makundi mengine yachukue ili kuleta maelendelo" alisema Meya Raibu
Lakini pia Meya Raibu amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhakikisha anaendelea kutoa elimu ya masuala ya fedha na ujasiriamali kwa wananchi ili kuwasaidia wananchi kutambua mahali sahihi pakuwekeze fedha hizo.
Akimaliza hotuba yake Meya Raibu amewataka wadau wote waliokabidhiwa kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya manispaa hiyo kuhakikisha kazi hiyo inamalizika kwa muda uliopangwa na sio kujificha kwenye msemo wa kazi inaendelea, bali wahakikishe wanatekeleza kauli mbiu hiyo ya kazi iendelee na ikamilike.