Tetesi: Meya wa Ilala aipa kampuni ya Kenya kazi ya kukusanya ushuru wa maegesho

Tetesi: Meya wa Ilala aipa kampuni ya Kenya kazi ya kukusanya ushuru wa maegesho

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Kazi ya kukusanya kodi za maegesho manispaa ya ILALA ambayo meya wake na naibu meya ni UKAWA wameipa kampuni ya Kenya airports parking service ya kenya ambayo haina usajili Tanzania.Hivi hizi kazi wazawa hawawezi fanya hadi apewe mkenya?
 
kazi ya kukusanya kodi za maegesho manispaa ya ILALA ambayo meya wake na naibu meya ni UKAWA imepewa kampuni ya Kenya airports parking service ya kenya ambayo haina usajili Tanzania.Hivi hizi kazi wazawa hawezi fanya hadi apewe mkenya?
Kama haina usajili Tanzania wamepewa vipi? Si ndiyo hao hao wapo Airport pia?
 
Penye rangi nyekundu ........una uhakika na hilo ?.
 
Wabunge wa CCM wapewa Rushwa ya Milioni kumi kumi hahahaha hio ndio inayohit Mpwa jiongeze
 
Lowasa angeshinda urais angeiuza hii nchi chapchap huku makamanda wanashangilia.
 
kazi ya kukusanya kodi za maegesho manispaa ya ILALA ambayo meya wake na naibu meya ni UKAWA imepewa kampuni ya Kenya airports parking service ya kenya ambayo haina usajili Tanzania.Hivi hizi kazi wazawa hawezi fanya hadi apewe mkenya?

Mkuu inabidi upanuke katika kufikiri kwako. Kwani kwa mfano, Swissport ni Watanzania? Sijui hata unajua Swissport ni kitu gani na inafanya kazi gani muhimu inayuhusu mabilioni ya fedha hapa nchini.

Hatuwezi tukawa tunaongelea kuongeza ufanisi wa huduma nchini na wakati huo huo tunataka tugawe kazi hata kwa watu wasio na sifa kwa sababu tu ni Watanzania wenzetu. Hiyo mentality ni ile ya wewe ukiwa kabila au dini fulani kuajiri watu wa kabila lako au dini yako tu, hata kama hawana sifa. Hujaona matokeo ya hilo hapa nchini? Muhimu zaidi kutumia soko la East Afrika. Kufikiri kwako kunaweza kusababisha hata huduma za mabasi ya abiria kati ya Dar es salaam na Nairobi ziwe zinaishia Namanga kwa kila upande.
 
kazi ya kukusanya kodi za maegesho manispaa ya ILALA ambayo meya wake na naibu meya ni UKAWA imepewa kampuni ya Kenya airports parking service ya kenya ambayo haina usajili Tanzania.Hivi hizi kazi wazawa hawezi fanya hadi apewe mkenya?

Ulitaka tenda wapewe mapadri na wachungaji wanaoficha meno ya tembo makanisani ???
 
Hiyo kampuni itakua ya mtu wa ukawa,kenya jina tu limewekwa hilo.
 
Penye rangi nyekundu ........una uhakika na hilo ?.

Ninauhakika hii habari sio tetesi naibu meya KATAMKA MWENYEWE KIPINDI CHA ASUBUHI RADIO ONE kuwa hiyo kampuni haijasajiliwa BRELA
 
Kama haina usajili Tanzania wamepewa vipi? Si ndiyo hao hao wapo Airport pia?

Hili ndilo linanishangaza hata mimi.WAliwapeje tenda watu ambao hawajasajiliwa BRela?
 
Ndio wanaokusanya airport pale na kwenye baadhi ya shopping malls ....wanafanya hivi bila kusajiliwa?
 
mshatoka kuchukua buku 7 naona mmevamia kufanya mashambulizi

habari hii ni ya uhakika sio tetei wala uzushi.Kampuni ya kenya imepewa soma hii habari

Halmashauri ya jiji Dar yajipanga kuzichukulia hatua kampuni zinazoitia hasara

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imesema haitomfumbia macho mtu, kampuni, wazabuni na makandarasi watakaolitia hasara jiji hilo hususani kampuni zilizopewa tenda za ukusanyaji mapato.

Pia imesema haitatoa tenda za zabuni kwa kampuni zisizokuwa na vigezo.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Meya wa Jiji hilo, Mussa Kafana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utendaji kazi wa kampuni tatu zilizoshinda zabuni za ukusanyaji kodi za maegesho katika halmashauri za manispaa zilizomo katika jiji hilo.

Amezitaja kampuni zilizoshinda zabuni hizo kuwa ni, Kenya Airport Parking Services katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Manispaa ya Kinondoni ilishinda Ubapa, wakati Temeke ikishinda kampuni ya Upauka.

“Tumechaguliwa na wananchi ili kuwaletea maendeleo ambayo yanatokana na mapato yanayokusanywa, hatotafumbia macho mtu yeyote atakayesababisha hasara au kuruhusu mianya ya upotevu wa mapato,” amesema.

Aidha, Kafana amefafanua utendaji kazi wa kampuni hizo baada ya kuwepo kwa malalamiko kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala haina mzabuni wa kukusanya mapato ya maegesho kutokana kwamba aliyeshinda tenda hiyo ambayo ni Kenya Airport Parking Services haijaanza kazi rasmi ya ukusanyaji kodi na kwamba huenda manispaa hiyo ikapoteza mapato.

“Kampuni hizi tatu zilikidhi vigezo, ambapo ya Kenya iliahidi kukuanya Bilioni 54 kwa mwaka na kwamba inatakiwa kukusanya milioni 20 kwa siku, ilitakiwa baada ya siku 28 ilete dhamana ya kazi ya asilimia 10 ya fedha ilizoahidi kutoa kwa mwaka ambayo sawa na bilioni 5.4, lakini hadi sasa haijatekeleza hilo na ndiyo sababu ya kutoanza kufanya kazi hadi sasa,” amesema.

Kafana amewatoa hofu wananchi juu ya hilo kwa kusema kuwa kampuni iliyomaliza muda wake imeombwa kuendelea kukusanya kodi za maegesho hadi pale halmashauri itakapotafuta mzabuni mwingine.

Kuhusu utendaji kazi wa kampuni nyingine zilizoshinda zabuni hiyo Temeke na Kinondoni, amesema zimeshaanza kufanya kazi.

SOURCE:Halmashauri ya jiji Dar yajipanga kuzichukulia hatua kampuni zinazoitia hasara - DEWJIBLOG
 
kazi ya kukusanya kodi za maegesho manispaa ya ILALA ambayo meya wake na naibu meya ni UKAWA imepewa kampuni ya Kenya airports parking service ya kenya ambayo haina usajili Tanzania.Hivi hizi kazi wazawa hawawezi fanya hadi apewe mkenya?

Wakenya wako juu zaidi yenu
 
Back
Top Bottom