Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Mhe Abdallah Mtinika amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kuipa hadhi ya kuwa Jiji Manispaa ya Temeke.
Mstahiki Meya ametoa ombi hilo leo mbele ya vyombo vya habari wakati wa baraza la Madiwani lililoketi kikao cha robo ya pili ukumbi wa mikutano wa Manispaa Iddy Nyundo.
Mhe Mtinika amefafanua kuwa Temeke ni moja kati ya Manispaa zilizoko katika Mkoa wa Dar es Salaam, na Ilala iliyopewa hadhi ya kuwa Jiji la Dar es Saalam mipaka yake iko wazi wote tunaifahamu.
“Sasa kama kigezo ni mapato na uwingi wa watu Manispaa ya Temeke inakidhi vigezo hivyo kwa kuwa mapato yake ni zaidi ya bilioni 36 kwa mwaka na idadi ya watu ni kubwa” Alisema Mhe Mtinika.
Aliendelea kusema kuwa ukiangalia majiji mengine kama Arusha , Mwanza na kwingineko Manispaa ya Temeke inazidi kimapato na hata idadi ya watu, na Temeke ikipewa hadhi ya kuwa Jiji itafanya vizuri zaidi katika nyanja anuai.
Sambamba na hilo Mstahiki Meya amesema Temeke tunasubiri kwa hamu awamu ya pili ya mradi wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam ( DMDP) kwa ajili ya kuendelea kuboresha miundombinu katika maeneo ambayo yamebaki na ametoa wito kwa wahusika kuhakikisha mradi huo usielekezwe sehemu nyingine kwa kuwa Temeke bado inauhitaji mkubwa na tayari waheshimiwa madiwani walisha wahaidi wananchi wanaowakilisha katika maeneo yao.
Aidha Mstahiki Meya amempongeza Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuapishwa kuwa Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumuhakikishia kumpa ushirikiano wa kutosha katika kulijenga Taifa la Tanzania.
... Jamhuri ya Muungano wa Tanzania…
Kazi iendelee...