Mfa maji haachi kutapa tapa

immasakha

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Posts
489
Reaction score
281
Michezo na Burudani
Manara awashtaki Yanga Mamlaka ya mapato’TRA’
December 31, 2018 Chumba-cha-Habari
Msemaji wa Klabu ya Simba, ambao pia ni Mabingwa Watetezi, Haji Manara amehoji Mamlaka ya mapato Tanzania juu utaratibu wa watani zao wa jadi kuhusu kuchangisha kwa ajili ya klabu yao na kuuliza kama utaratibu huo ni sahihi.

Manara amehoji iwapo kama Klabu hiyo inayoongoza msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara kama inalipia kodi katika Mamlaka hiyo huku akisistiza kwamba hata kama ukweli ukiwa mchungu kiasi gani lazima usemwe.

“TRA nakumbuka mlienda katika kanisa la Mchungaji Kakobe kufuatilia ile michango na zile sadaka za waumini, Vipi kwa hawa wanaochangisha kila uchwao? wana mashine za EFD? wanalipia kodi za hizi Rambirambi za kujitakia?”, ameandika Manara.

“Nategemea ‘soon’ (mapema) wahusika watatoa maelekezo sahihi ya huu utamaduni unaotufedhehesha Watanzania na ambao ukiachwa unaweza kusababisha kizungumkuti cha kukokotoa hesabu”. Manara amesema katika kusisitiza kauli yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…