Mfadhili Kikwete...

Makaayamawe

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2009
Posts
341
Reaction score
9
Raisi wetu inaelekea yuko busy kweli kweli. Hapa anashughulikia sera ya kugawa pikipiki. Natumaini walemavu wote nchini watapewa angalau pikipiki moja-moja. Kweli tunaye rais.



PRESIDENT Jakaya Kikwete (third right) chats with a woman with a physical disability, Sara Mageni Sanga (sitting down), of Lupalilo village in Makete District, Iringa Region, after presenting her with a Bajaj auto rickshaw today to facilitate her movement. Looking on, second right, is the Iringa Regional Commissioner, Mr Mohamed Abdulaziz. (Photo by Freddy Maro).
 
Wizi mtupu. Nimfadhili nini. Aende kwa Obama kama anataka ufadhili, Bush ashatoa vyandarua Obama labda atampa more Bajaj.
 
wewe ndio unajua leo tunaye...
 
Sawa Mkulu kamfadhili huyo mama hiyo Bajaj; Je amemfanyia mpango wa kupata mafuta ya hiyo Bajaj? Inavyoelekea huyu mama hana uwezo wa kumudu kununua petrol ya hiyo bajaj kwa hiyo pengine ile ya miguu mitatu ya kusukuma kwa mikono ingemfaa zaidi!! Just thinking aloud.
 
Imekaa kama photo opportunity kuelekea 2010. Kwani kuna wtz wangapi wenye ulemavu na hali ngumu kama huyu mama? Ktk hiyo miaka minne amewawekea mikakati gani zaidi ya kabajaji hako?
 
yaani huyu hana habari kabisa kuwa huku nyumba inaongua na maamuzi yake ya IPTL..daaah tutajuta kumfahamu huyu
 
Bajaj hii lazima mhindi katoa na JK yeye anachukulia ujiko tu hapo . Nchi hii ina mazingaombwe jamani .
 
"Inavyoelekea huyu mama hana uwezo wa kununua petrol" WEWE WASEMA. Kwa kigezo gani unamuhukumu? Au ni huo udhaifu wake? Nakusihi umuombe radhi huyo mama tafadhali.
 

Kabla sija kubali kuwa tunaye raisi kweli nabidi niulize. Hizo piki piki zime tolewa na nani? Serikali au wafadhili? Maana kama yeye jukumu lake peke lilikua kwenda kutoa hizo piki piki hapo haja fanya kitu.
 
"Inavyoelekea huyu mama hana uwezo wa kununua petrol" WEWE WASEMA. Kwa kigezo gani unamuhukumu? Au ni huo udhaifu wake? Nakusihi umuombe radhi huyo mama tafadhali.

Alibaba mkuu heshima mbele, sina haja ya kumuomba radhi huyo mama kwani nilichosema ni sahihi na punde si punde itadhihilika hivyo!! Nayafahamu mazingira ya huko Makete!!
 

Mama kapewa Bajaj, je atapelekwa shule ya udereva na je leseni ya kuendesha atakuwa nayo, au kwa sababu yeye ni mlemavu, basi sheria haitambana.
 
yaani huyu hana habari kabisa kuwa huku nyumba inaongua na maamuzi yake ya IPTL..daaah tutajuta kumfahamu huyu

Yeye ni wa kamera tu. Bajaj atawapa walemavu wangapi na kwa pesa ya nani? Watu hata milo miwili hawana yeye anafuja pesa kwenye bajaj. Bado kidogo nchi itakuwa gizani na bila aibu tutamuon akipanda ndege kwenda shopping NY, USA.
 
kama ana uwezo mbona alisubiri miaka yote akijivuta chini mpaka apewe ya bure? Kwa simple mind lazima ujue tu kwamba hana hela na mafuta itamwia shida tu.

Hawana tofauti na Ludenga anayetoa gari la shilingi milioni 30 kwa kabinti kanafunzi. Pesa ya mafuta itabidi aipate kwa kujiuza au auze gari baada ya muda mfupi!
Hii ndio bongo bwana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…