Teko Modise
JF-Expert Member
- May 20, 2017
- 2,331
- 7,733
Hayati Michael Jackson enzi za uhai wake alikuwa ni mwingi wa vituko huko Hollywood.
Ukitazama Video ya Kibao cha Liberian Girl ya kwake hayati Michael Jackson utamuona sokwe Bubbles miongoni mwa mastaa wa miaka ya 1980 waliohudhuria video hiyo.
Sokwe huyo wa kiume anajulikana kama Bubbles aliyepata kufugwa na Michael Jackson enzi za uhai wake.
Sokwe huyo ni miongoni mwa Sokwe wachache sana duniani kula bata la nguvu na kuishi maisha ya kifahari pengine hata kuzidi binadamu tunaoishi huku kwenye dunia ya tatu.
Sokwe Bubbles alizaliwa mwaka 1983 na kununuliwa na mwanamuziki Michael Jackson (MJ) kutoka kituo cha utafiti wa Wanyama huko Texas, Marekani.
MJ akaanza kusafiri maeneo mbalimbali ya dunia akiwa na Bubbles na kuibua hisia tofauti tofauti kwa wadau wa muziki.
Bubbles alitunzwa kwenye nyumba ya familia MJ mpaka mwaka 1988 alipohamishiwa kwenye hekalu binafsi la MJ la Neverland Ranch kule California.
Bubbles akawa analala kwenye chumba cha MJ, akawa analishwa kwenye dining table ya MJ, kuvalishwa diaper na ikafika mbali zaidi hata kutumia choo cha MJ na inasadikika kuna mtu aliajiriwa kwa ajili ya kuhakikisha Bubbles yuko smart muda wote yaani kumbadilisha diaper, kumuogesha, kumvalisha nguo nk.
MJ akawa anamtoa Bubbles out na kumpeleka katika migahawa mikubwa Marekani, sehemu za Fukwe mbalimbali nk
Kuna wanaosema, MJ alimtafutia Bubbles mlinzi binafsi (bodyguard) pamoja na Wakala.
Vituko vya MJ na Bubbles vilifika mbali kwani Bubbles alipata fursa ya kuhudhuria zoezi la kurekodi albamu ya MJ iliyoitwa Bad ya Mwaka 1987 na Bubbles akapata fursa ya kushiriki tukio la ku-shoot video ya Liberian Girl na akatajwa kama mmoja ya wageni waalikwa wa Video hiyo, uthibitisho upo tafuta Video hiyo itazame mpaka mwisho utathibitisha.
Alipokuwepo MJ basi ujue Bubbles yupo kando yake na uangalizi wa asilimia 100 toka kwa wapambe wa Michael Jackson (MJ).
MJ akaamua kuitangaza albamu yake kwa kuandaa show nchi mbalimbali duniani na kuiita “Bad world tour” na kupitia tour hiyo, vituko vyake na Bubbles vikazidi.
Katika jiji la Tokyo, walilala chumba kimoja cha vitanda viwili kwenye hotel ya nyota tano na kesho yake kwenda kumtembelea Meya wa Jiji hilo na kunywa naye chai, tukio lililowaacha wengi midomo wazi. Meya wa jiji hilo akaishia kumsifia kama rafiki mwema. Ikawa ni mara ya kwanza kwa mnyama kuruhusiwa kuingia ofisini kwa Meya🤣
Bubbles akakutana na kizingiti cha kuingia Uingereza pamoja na Sweden kwasababu ya sheria mbalimbali. Lakini haikuwa kesi maisha yakaendelea.
Bubbles amehudhuria sherehe nyingi na kukutana na mastaa wengi kama vile Promota maarufu wa ngumi Don King, Elizabeth Taylor aliyekuwa best wa MJ, Kenny Rogers, na wengineo wengi.
Mwanamuziki Freddie Mercury aliwahi kukasirishwa na tabia ya MJ kwenda na Bubbles studio na kuhoji ukaribu wa wawili hao huku akitishia kuacha kufanya kazi na MJ. Dunia ikabaki na maswali mengi kuliko majibu juu ya mahusiano ya MJ na Bubbles.
Mwaka 2005, Bubbles akazidi kuwa mkubwa kimwili huku MJ akiwa anategemea kupata mtoto wake wa kwanza na kwa usalama wa mtoto wake huyo, akaamua kuacha kuishi na Bubbles katika jumba lake.
Bubbles akahamishiwa na kwenda kutunzwa huko Center for Great Apes huko Florida na kuendelea na maisha yake mpaka leo.
MJ akiwa na mwanae aliwahi kwenda kumtembelea Bubbles mara moja tu. MJ aliwahi kusema alimchukulia Bubbles kama rafiki yake na mwanae lakini pia yeye anapenda kujihusisha na wanyama tofauti na watu wengi walivyokuwa na mtazamo hasi.
MWISHO.