Mfahamu Captain/Master, Pilot , Tug Master, Boatman, Coxswain, Skipper na Helmsman.

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2018
Posts
5,489
Reaction score
14,091
Captain/Master
Huyu ni baharia au mfanyakazi wa meli mwenye leseni kubwa ya uendeshaji wa meli. Ndiye msemaji na kiongozi mkuu mwenye kutoa amri katika meli.
Pia ni anamuwakilisha mmiliki wa meli popote meli ilipo.

Pilot
Huyu ni mtu mwenye leseni na ujuzi wa kuongoza meli ambaye anafanya kazi ya kuingiza na kutoa maelekezo meli inapoingia bandarini.

Sifa kuu ya pilot ni kuwa na ufahamu mkubwa wa eneo hilo la bandari, kuhusu kina cha maji,miamba na mawimbi.

Meli inapotaka kuingia bandarini yeye huenda kuifata nje au nangani na kumpa oda Captain wa meli mpaka anapofika kwenye kupaki katika gati.
Kwenda kuifata meli huwa anatumia boti ndogo inayoitwa Pilot Boat na hupanda kwenye meli kwa kutumia ngazi ambayo huitwa Pilot Radar na hupokelewa na mtu ambaye ameandaliwa ampeleke sehemu ya kuongozea meli.

Tug Master
Huyu ni mfanyakazi wa bandari ambaye ni baharia mwenye leseni ya kuongozea meli. Ambaye shughuli yake ni kusaidia kusukuma au kuvuta meli kubwa inapotaka ipaki au itoke eneo la bandari kwa kutumia Tug (Boti ndogo yenye nguvu).

Kwenye kuvuta hutumia kamba maalum ambazo hufungwa kati ya Tug na Meli. Na kusukuma hutumia sehemu ya mbele ya Tug na katika melo kuna maeneo maalum ya kusukuma yameandikwa Tug.

Ukiwa eneo la bandari unaweza ukaona kuna boti ndogo moja au mbili zinakuwa kando ya meli kubwa.

Boatman
Huyu ni mwendesha boti au chombo kidogo. Mfano anayeendesha boti kwa ajili ya utalii, kupeleka mahitaji au boti ya kufungia kamba (Mooring Boat).

Coxswain
Huyu anaendesha boti au chombo kidogo pia ana leseni ya kuongozea vyombo vya majini.
Mfano wa Coxswain ni yule anaendesha Pilot Boat.

Skipper
Huyu ni baharia anaye endesha au kuongoza chombo kidogo cha majini. Skipper huwa sana hutumika kwa waongoza vyombo vya uvuvi, starehe au boti zisizo za kibiashara.
Kwa baadhi ya nchi huwa na leseni zao kulingana na uwezo wa abiria na chombo.

Helmsman
Huyu ni baharia wa kawaida katika meli ambaye kazi yake ni kushika usukani.
Huwa na cheti cha Able Seaman ambacho kinamuwezesha kuwa zamu endapo chombo kinatembea (Navigation watch).

Kipindi cha nyumba kabla ya teknologia kukua hawa washika usukani walikuwa ni watu waliojazia sana kutokana na meli kuwa na usukani (Steering) ambazo zilikuwa ngumu na kubwa sana.

Ndio maana ilikuwa ukimuona mshika usukani anakuwa ni mtu wa nguvu.
Lakini sasa kuna usukani za kisasa ambazo ni laini kama wheel( usukani ya tairi au mduara ambazo ni ndogo) kuna joystick na button.
 
Weweni nani kati ya hao,ongezea tupicha mkuu mbona mchoyo hivyo kwani umekua ugali huo
 
Write your reply...anayeendesha nyambizi nae nasikia ni skipper ufafanuzi tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…