Basi Nenda
JF-Expert Member
- Jul 29, 2017
- 20,774
- 47,866
Jina kamili aliitwa Francois Duvalier. Alizaliwa 14 April 1907 na kufa 1971. Alikuwa rais wa Haiti 1957-1971
KABLA YA URAIS
Alipata degree ya madawa Chuo Kikuu cha Haiti 1934 na baadae kama daktari hospitali mbalimbali. 1946 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa huduma za afya za taifa, 1949 akawa Waziri wa Afya.
URAIS
Katika kampeni za 1957 aliahidi kuijenga Haiti na wananchi wa Haiti wa vijijini walimsapoti sana na Jeshi pia. Haiti kwa kipindi kirefu ilitawaliwa na mullato(wahaiti weupe). Alichaguliwa kuwa raisi 1957
WEHU
Mnamo tarehe 24/5/1959 alipata shambulio kubwa la moyo na kubaki hajiwezi kwa masaa 49. Wakati akiwa akipona taratibu aliiacha nchi kwa Clement Barbrot lakini alipopona akadai Clement alipanga kumpindua hivyo akamfunga.
Clement aliachiwa 1963 na kuanza kupanga kumpindua Duvalier. Akaanza kwa kumtekea watoto, ikashindikana hivyo Duvalier akagundua na kuagiza Clement asakwe nchi nzima. Katika msako Duvalier akaambiwa Clement kimiujiza kajigeuza kuwa mbwa mweusi, akaagiza mbwa wote weusi Haiti wauawe.
Clement alikuja kukamatwa na kuuliwa na Duvalier akaagiza kichwa chake kiwekwe kwenye barafu apelekewe ili wafanye mazungumzo.
SHAMBULIO LA KUMUUA
1967 mabomu yalilipuka nje kidogo ya ikulu ya Haiti, Duvalier akaagiza walinzi 19 wa kikosi cha rais wauawe.
Baada ya siku chache akiwa kwenye hotuba akatoa karatasi ya majina ya wale walinzi wake 19 alioagiza wauawe, akasoma jina moja moja kwa sauti na kujibu 'HAYUPO' baada ya majina yote akasema 'WOTE WALIPIGWA RISASI'.
CULT OF PERSONALITY
Duvalier aliagiza picha kubwa ya Yesu ichorwe na kuwekwa mtaani ambapo ilionesha Yesu akimshika bega Duvalier na kusema 'nimemchagua'.
KIFO CHA KENNEDY
1963 baada ya kifo cha rais wa Marekani, JF Kennedy, Duvalier alidai yeye ndiye alisababisha kwani alimpa laana Kennedy
HATMA YAKE
Alikufa 1971 na kumuachia madaraka mwanaye wa pekee aliyeitwa Baby Doc(hii ni a.k.a).
Utawala wa Papa Doc ulisababisha vifo vya Wahaiti 60,000.