Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 122,494
- 96,074
MFAHAMU DIKTETA WA MALAWI ALIYEPIGA MARUFUKU KUVAA SURUALI
Baba wa Taifa la Malawi, Dikteta Hastings Kamuzu Banda aliingia Malawi mwaka 1958 akitokea Uingereza alikoenda kusoma tangu 1925, alianza harakati za kudai Uhuru mwaka 1957 na Malawi ikapata Uhuru 1961 yeye akawa Raisi na kutangaza kuwa Raisi wa Malawi kwa Maisha yote.
Alitangaza mambo mengi kuwa marufuku Malawi, kwa mfano wanawake kuvaa suruali, kuonyesha magoti , wanaume kuwa na nywele ndefu au suruali fupi. Makanisa yalipaswa kutafuta kibali cha serikali, Mashahidi wa Yehova walipigwa marufuku.
Mwaka 1983 aliwaua mawaziri watatu waliokuwa wanamwambia kuhusu mfumo wa vyama vingi, alipowaua akawaweka kwenye gari gari hilo likisukumwa kwenye korongo . Radio Malawi ikatangaza Mawaziri wanne wafariki kwa Ajali baada kutumbukia kwenye Korongo. Raisi Kamuzu akaamuru wazikwe siku hiyo hiyo miili yao isioneshwe kwa kuwa imeharibika.
Mwaka huo huo alitimua Wabunge wote wa Bunge la Malawi kwa amri yake wakawa sio Wabunge tena, Alitangaza kila Mwananchi hadi watoto wawe na kadi ya chama chake cha MCP asiyekuwa na Kadi hakuruhusiwa kupata huduma muhimu mfano Matibabu, Shule, nk.
Alipiga marufuku upinzani nchini humo akidai ata Mungu alikuwa hataki upinzani ndio maana alimfukuza Shetani.
Kamuzu alikuwa anatembea na Fimbo mbili moja yenye manyoya kwa ajili ya kufukuzia Nzi akidai UK hakuwahi kuona nzi. Kamuzu hakuwahi kuoa bali alikuwa anaingiza wanawake tofauti tofauti Ikulu.
Hadi Oktoba 1992 Banda alipaswa kukubali kura ya wananchi kuhusu swali la kukubali vyama vingi baada ya Maandamano nchi nzima wakiwemo Wanajeshi na Polisi
Kura hii ilileta asilimia 64 kwa ajili ya demokrasia ya vyama vingi . Mwaka huohuo halmashauri mpya ilitangaza
katiba mpya na kuondoa "urais wa maisha".
Katika uchaguzi wa mwaka
1994 Banda aligombea tena Urais lakini alishindwa na Bakili Muluzi . Chama kipya cha Muluzi kilipata wabunge wengi.
Banda aliendelea kuwaangalia Wamalawi kama "watoto wa siasa" akatabiri ya kwamba wanahitaji "mkono wa chuma".
Mwaka 1997 alingonjeka akapelekwa kwa matibabu Afrika Kusini alipofariki tarehe 25 Novemba 1997 akiwa na
umri wa miaka 99
Huyo ndiye Kamuzu Banda aliye jitangazia kuwa ni rais wa maisha wa Malawi kwa ulevi tu wa madaraka.