Mfahamu Howard Stern: Mtangazaji Tajiri zaidi Duniani

Dira...
Nilidhani kuwa unataka tufanye mjadala wa kuheshimiana.
Mimi mjadala huu uliokujanao hapa wa kunikejeli huwa sijibu.

Hapa tulipofika panatosha.
Mzee Wangu uyo kijana nadhani alileta ki-utani TU, usiichukulie too serious.

Maana comment yako khs Sykes na TANU imeanzisha mada ndani ya mada[emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dira...
Nilidhani kuwa unataka tufanye mjadala wa kuheshimiana.
Mimi mjadala huu uliokujanao hapa wa kunikejeli huwa sijibu.

Hapa tulipofika panatosha.
Mzee wangu watu wanaku-missjudge mno humu sijui kwanini. Mimi si muislam lakini mpenzi sana wa historia (japo ni mwanasayansi) lakini napenda kujua ukweli kuhusu mambo mengimengi hata kama si ya kweli.
Nimekufatilia sana ninapopata mida na nilifurahi kukusikia na kukuona kwenye kipindi cha Zumari cha UTV, nilifaidi sana.

Tafadhali usivunjike moyo.

Bado tupo tunaopenda kupata kujua mambo yalivyokuwa hapo zamani.
 
Possibles,
Mimi siwashangai na nawaelewa vyema kabisa.

Makala yangu ya kwanza ''In Praise of Ancestors,'' Africa Events (London) 1988 nilimtaja Abdul Sykes kama muasisi wa TANU na nikaitaja Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Toleo zima lilikusanywa.

Leo hawa ndugu zangu akili zao zinakataa kuamini kuwa historia waliyosomesha kwa zaidi ya nusu karne haikuwa sawa.

Hawakuelezwa kuwa katika TANU kulikuwa na Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Suleiman Takadir akiwa Mwenyekiti wa Baraza la TANU.

Akina Rugambwa walikuwapo lakini walijiweka mbali sana na harakati za kupigania uhuru wakati Sheikh Hassan anauza kadi za TANU misikitini.

Hawakuelezwa kuwa Ally Sykes alikuwa na kadi no. 2 na kadi no. 3 ni ya kaka yake Abdul Sykes.

Iweje iwe hivi?

Leo wanashangaa kwa nini kila nikiandika historia ya TANU Sykes hawakosi.
Wanadhani nawapenda tu.

Na kubwa linalowatesa ni kule kusoma majina ya Kiislam katika historia nzima ya kudai uhuru.

Lakini huu ndiyo ukweli wenyewe.
Mimi si mtu wa kuvunjika moyo toa hofu.
 
Asante sana mzee, kama kuna kitu cha kujivunia sisi vijana waleo ni wewe. Bahati mbaya nyakati tulizonazo leo hii sio rafiki kwa historia kwa sababu vijana wengi wako na mwelekeo wa maudhui mengine ya kiburudani zaidi haswa mada kama hizi tunamojadiliana sasa.
Lau ingengekua ni mada nyingine ya kihistoria nikiri tu nisingejua haya ulio yawasilisha hapa.

Maadamu maandishi hayafutiki kwa wepesi mimi nakuombea heri mzee kwa majitoleo yako kutujulisha haswa historia ya nchi na taifa letu kinyume na tulivyo kua tume ambiwa.
 
Mzee wangu hata mimi mwanzoni nilipenda sana threads zako ila nikaona umejaa sana udini na hao kina Sykes unawatumia tu kwenye agenda yako ya udini. Ila bado una nafasi ya kuandika thread zisizokuwa na udini.
 
Mzee wangu hata mimi mwanzoni nilipenda sana threads zako ila nikaona umejaa sana udini na hao kina Sykes unawatumia tu kwenye agenda yako ya udini. Ila bado una nafasi ya kuandika thread zisizokuwa na udini.
Dira...
Kutofautiana ni silka ya ubinadamu.

Inawezekana kwako kwa kuwa mimi nimeandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na ukasoma majina mengi kuwa ni ya Waislam ukaona huo ni udini.

Lakini ushajiuliza kwa nini historia hii ilifutwa?

Yawezekana kufutwa kwake ni kwa kuwa waandishi waliona historia ya uhuru imejaa Waislam wengi?

Ushajiuliza kwa nini historia hii ilifutwa?

 
Penda...
Ahsante sana.
 
Another day in Paradise!Wazungu wamejawa na vibweka sana.
Moise...
Phil Colllins, ''Another Day in Paradise.''
Umenikumbusha mwaka wa 1990 niko ndani ya Machava Stadium, Maputo.

Yvonne Chakachaka amekuja Maputo na bendi yake na anafanya show Machava Stadium.
Bahati nzuri kafikia hotel niliyokuwa nimepanga inaitwa, Cardoso.

Miaka ile hii ilikuwa hoteli ya pili kwa uzuri ya kwanza ni Polana.
Nimekwenda kutazama show yake.

Uwanja umefurika.

Kabla ya Yvonne Chakachaka kupanda kwenye stage walikuwa wanapiga nyimbo za Temptations na Phil Collins, ''Another Day in Paradise.''

Nina stori ndefu na Yvonne Chakachaka.
Ikapita miaka tukaja kuonana Arusha yeye akiwa Ambassador wa Roll Back Malaria.

Nikamkumbusha ile show yake ya Maputo.
Akaniuliza ulikuwako Machava Stadium siku ile?

Nikamjibu, ''Naam na tulipanga hoteli moja.''
Nikamuuliza, ''Haya imekuwaje mbona umekuwa mnene hivi?''y

Akacheka sana akaniambia, ''Nimeolewa na nina watoto.''

Mnisamehe ni nje ya maudhui iliyopo mezani lakini ''Another Day in Paradise,'' miaka 32 iliyopita nimekumbuka mbali sana.


Yvonne Chakachaka Arusha 2008
 
Naam.Ni wimbo mzuri sana mkuu.
 
Nimefatilia japo kwa kiasi kidogo historia ya nchi nyingine duniani hasa Ulaya. Hawaelezi jinsi walivyokuwa na mapigano ya ndani kwa ndani kwenye kujipatia uhuru na pengine kuangusha tawala mbalimbali.

Japo kwetu Africa napo wamejitahidi kuonyesha kuwa tumekuwa tukiuana mno kwa uchu wa utawala.

Hizo aya mbili hapo juu zinaonyesha kabisa wenzetu hawa wa Ulaya ni mabingwa wa kupindisha na hata kuchezea history ili iandikwe kwa namna wanayotaka wao.
Hakuna kosa kabisa historia yetu ikaandikwa bilevile ilivyotokea. Na namna pekee ni kwa kupata masimulizi ya waliokuwepo, vitabu, majarida na maandiko kutoka kwa walioshiriki na kushuhudia.

Inaniuma sana ninapoona mwafrika/mtanzania mwenzangu anapoogopa kuijua historia ya nchi bara/nchi yake kwa kuhofia majina flani au dini. Ni tabia mbaya kuuhofia ukweli.

Kwa mfano mpaka leo sijui Mzanzibari mzawa/halisi ni nani. Ni kabila gani? Muasisi wa taifa la Zanzibar Karume ni mzanzibari halisi?

Nilipata kuona picha za waziri mkuu wa kwanza wa Zanzibar akiwa UN. Hizi nchi mbili (Tanganyika na Zanzibar na hatimaye Tanzania) zina historia kubwa ambayo ikiwekwa vizuri ni faida sana kwa vizazi vyetu na vijavyo.

Hivi lakini hii taaluma yako kuna mtu unamrithisha? Una mpango wowote wa kuihifadhi electronically maana vizazi vijavyo sidhani kama vitatumia sana vitabu na shelves kupata taarifa za kale.
 
Possibles,
Hili la kurithisha sijaelewa narithisha kitu gani?

Kuhusu kuhifadhi historia hii ni kuwa vipo vitabu na paper nilizoandika katika mtandao halikadhalika kuna audio na video.

mohamedsaidsalum.blogspot.com
mohamedsaidsalum.com
 
Possibles,
Hili la kurithisha sijaelewa narithisha kitu gani?

Kuhusu kuhifadhi historia hii ni kuwa vipo vitabu na paper nilizoandika katika mtandao halikadhalika kuna audio na video.

mohamedsaidsalum.blogspot.com
mohamedsaidsalum.com
Hizo link tayari ni namna ya kupata urithi wa taarifa ulizonazo kwenye kumbukumbu zako.

Ahsante.
 
Hawakufanikiwa kuzaa na huyo demu mweusi
 
Hicho kitabu "the life and times of A. Sykes " kinapatikanaje? Nimetafuta mtandaoni bila kufanikiwa.
 
Hawakufanikiwa kuzaa na huyo demu mweusi
Hawakufanikiwa mkuu,
Hayakua mahusiano serious kivile,
Nnahisi walikua kwenye zone ya friends with benefits
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…