Mfahamu Hussein Shekilango, aliyepewa barabara Dar (Bamaga - Urafiki) kutambua mchango wake kwa Taifa

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952

Hivi kuna yeyote amewahi kujiuliza Shekilango ni nani mpaka barabara kubwa jijini DSM ikapewa jina lake?

Naomba mwenye historia na wasifu wa Shekilango atuwekee. Naamini siko peke yangu ambaye hatuna taarifa zake.

=====

Michango ya wadau...


 
Ninachokumbuka alikuwa waziri na alikufa akiwa njiani toka Uganda kwenye ajali ya helkopta, hivyo alikufa akiwa kazini enzi za mwalimu, baada ya vita vya kumuondoa Nduli Iddi Amini.
 
Halafu haya majina ya Shekilango na Shemhando ni hayo hayo ya Kilango na Mhando

wasambaa zamani walikuwa wanafikiri mtu kuitwa sheikh ni title ya ujiko
so wakaanza kuongeza sheikh kwenye majina yao.

Yaani mhando ikawa sheik mhando
kilango ikawa shekilango
lukindo ikawa shelukindo n.k

sasa ndo imekuwa hivyo.
 
Alikuwa Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu na alifariki 1980 akitokea Entebbe Uganda, na ndege iliangukia Arusha, unaweza kusearch Hussein Shekilango nafikiri unaweza kupata data zaidi.
 
..hivi kuna yeyote amewahi kujiuliza Shekilango ni nani mpaka barabara kubwa jijini DSM ikapewa jina lake?

..naomba mwenye historia na wasifu wa Shekilango atuwekee. naamini siko peke yangu ambaye hatuna taarifa zake.


Kaka Joka Kuu,

Mzee Hussein Shekilango aliwahi kuwa Mbunge wa Korogwe na Baadaye alikuwa waziri Wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu anayeshughulikia mambo ya Utawala (Nafikiri utakuwa unawafahamu watumishi wa namna hii).Mzee Shekilango alikuwa mtu wa karibu sana na Rais Nyerere (RIP) na Waziri Mkuu wa wakati huo Mh.Edward Sokoine (RIP).

Ilikuwa mwezi May/1980 Mzee Shekilango pamoja na watumishi wengine wa serikali na Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi walipata ajali ya ndege huko Arusha na kufariki.Mzee Shekilango na ujumbe wake walikuwa wanasafiri kwa ndege ndogo kutoka Arusha kwenda Entebbe.Ikumbukwe kuwa kipindi hicho tulikuwa katika vita na Utawala wa Amin,na inasemekana Mzee Shekilango alikuwa ametumwa na Rais kwa kazi maalumu huko Uganda.

Sina Ufahamu ni nani alipendekeza Jina la Barabara ile ya Shekilango (Mwenge/sinza) lakini Shekilango anahesabiwa kama shujaa,kwa sababu alikufa kazini na katika shughuli za Vita vya Kagera.Mtoto wa Kiume wa Marehemu Shekilango alikuwa mmojawapo ya wanachama wa CCM 19 walioomba Ubunge wa Korogwe -Magharibi katika Uchaguzi Mkuu wa 2005.
 
Wow this is interesting i never though ile barabara ya shekilango imewekwa kutoka na umaarufu wa mtu. Nimefurahi kujua hii
Bravo aliyeleta hii mada!
 
Ukitaka kujua zaidi nenda Sea View, mama Shekilango yupo huko.
 
The Boss,

Hey The Boss,
My mom is msambaa and my daddy is half Irish half dutch.

Taarifa yako sio ya kweli.
Wako watu wanaitwa Lukindo mpaka leo, and what I can remember is that, Lukindo is called Ukindo in Kisambaa
Wako watu wanaoitwa Kilango mpaka leo.

She in kisambaa is [ a son of ]

See this, Maukindo
A daughter of Ukindo.
 
The Boss,

Mkuu,

Huu ndio twaita ubahau. Ujifunze kwa kutaka kujifunza hasa.

Uende taratibu mkuu.
 

Mkuu Wasambaa tulikua tuna weka "she" siyo "sheikh". Na huko kuweka "She" ni kwa mtu ambae anaoa msambaa. So Mhando akimuoa msamba inawekwa "she" anakua Shemhando.
 
Mie hapa nashangaa kumbe kila kitu kina maana yake. Na Mandela Road, Samora zina maana gani?
 
Mh bibie hata hizi nazo?

Hizo nimeuliza kwa nini ziliitwa hivo

Hiyo Mandela ni rais wa SA alikuja TZ wakaita barabara Mandera Or

Na Samora - Ni Sababu Ya samora wa Msumbiji or kuna maana nyingine

aulizae ataka kujua ??🙂nijibu basi kimei mie niko huku Bariadi village kwa kina Kanumba
 
Hizo zote ni Heshima Waliopewa hao wa asisi wa mataifa ni kuwaenzi wapigania Uhuru ndo maana hata ukienda Zimbabwe, Namibia, kuna nyerere road huko! by the way Bariadi village hakuna salooni inayoweza kutengeneza unywele huo bibie! teh teh
 
Hizo zote ni Heshima Waliopewa hao wa asisi wa mataifa ni kuwaenzi wapigania Uhuru ndo maana hata ukienda Zimbabwe, Namibia, kuna nyerere road huko! by the way Bariadi village hakuna salooni inayoweza kutengeneza unywele huo bibie! teh teh

Thanks u make ma Nyerere Day
 

Mkuu Wasambaa tulikua tuna weka "she" siyo "sheikh". Na huko kuweka "She" ni kwa mtu ambae anaoa msambaa. So Mhando akimuoa msamba inawekwa "she" anakua Shemhando.

Mhando
Kilango au kisambaa chenyewe( Kiango)

Na hii yote ilitokea wakati huo wa enzi za mababu kwamba mtoto wa Kiango anaweza kuitwa Shekiango
Au hata kuoa tena, mwanaume akioa anaweza kuchukua title ya mke wake.

Kama mwanamke ni Mzingwa basi mwanaume atakayemuoa anaweza kua akachagua jila la Shemzigwa.
As my mom said, She = son of or mume wa...

Kama Yugoslavia wanavyoitana Milosovic, Ibrahimovic.

Wanaojua kisambaa zaidi wafafanue, kwani mimi haya nilifundishwa na mama labda kuna Ufafanuzi zaidi
 
Marehemu shekilango alifariki 19 may, 1979, nikiwa darasa la tano, one of our relative luteni peter mallya died in that accident, ndege iligonga vilima fulani huko arusha kutokana na hali mbaya ya hewa.

Luteni Mallya, our relative was the only son to his parents.

Siku hiyo gazeti la Uhuru liliandika shekilango na wengine sita wafariki
 
duh! nimeiona hii leo, historia ya shekilango niliwahi kuambiawa kuwa, enzi hizo huyo mzee shekilango alikuwa anaishi sinza, kwahiyo wasambaa wakiwa wanasafiri kuja dar walikuwa wanasema kwa kisambaa ''TITAITA KWA SHEKIANGO'' yaani tunakwenda kwa mzee shekilango, so ikawa kila mtu anasema anakwenda kwa shekilango na ndio ikawa mwanzo wa shekilango na hatimaye hiyo barabara ikapewa hilo jina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…