Masiya
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 7,602
- 7,332
Ikiwa kesho ni Valentine's day nimeona niwaletee taarifa kuhusu mtajwa hapo juu alie zaliwa siku hiyo ya Valentine.
Joseph Kiambukuta Londa a.k.a Josky, Josky Kiambukuta, Djoe Sex, Le Commandant de Bord alizaliwa mjini Kinshasa February 14, 1949 (Siku ya Valentine). Akiwa na miaka 15, 1964 alitunga nyimbo na kumpelekea Lutumba Simaro wa OK Jazz ambae baada ya kusikiliza alimwambia kijana endelea tu na utunzi wako iko siku tutakuwa pamoja.
Akiwa na miaka 20, 1969, alifuatwa na washikaji wa Dr. Nico Kasanda na kuombwa kujiunga na bendi ya African Fiesta Sukisa kujazia safu ya waimbaji yeye akiwa na sauti ya “Tenor” iliyokuwa ikisakwa na Dr Nico. Akiwa hapo aliimba nyimbo kadha na kutunga za kwake. Msikilize hapo chini akishusha vitu.
[Sadi Motema]
Ikumbukwe yakwamba Josky kama tenor alihusudiwa sana na Grand Kalle wa African Jazz « Baba wa Muziki wa Kisasa wa DRC » kama alivyoimba Tabuley na Franco kwenye Lisanga ya Banganga (1983) na ushiriki wa Josky.
Mwaka 1971 kwa msaada wa Master Tauris Ngombe na mkewe Mama T Ngombe pamoja na Mama Mobutu wapigaji kadha wa African Fiesta Sukisa na bendi nyingine walianzisha bendi yao ya L’Orchestre Continental. Josky kiambukuta aliletwa na Bopol Mansiamina waliokutana kwa Dr. Nico na Josky akawa mwimbaji sauti ya kwanza pamoja na Wuta Mayi na Tino Mwinka. Kibao chake kimoja ni hiki cha Nakobondela.
[Nakobondela bolingo]
Mwaka 1972 bendi ile ilisambaratika inasemekana Franco, Tabu Ley na Verckys walikuwa wahusika wakubwa na Josky alikuwa katikati ya mipango ya kujiunga na bendi ya Rochereau ya African Fiesta. Mwaka huo bendi ya TP OK Jazz iliamua kimkakati kuchukua waimbaji wa shule ya “African Jazz” na wakwanza alikuwa Sam Mangwana. Simaro Lutumba alimtafuta Josky na kumuambia nyumbani kwake ni TP OK Jazz na January 1973 Josky alitua rasmi TP OK Jazz ambako alidumu hadi December 1993 bendi ilipovunjika. Baada ya muda si mrefu alikuwa mwimbaji wa kutegemewa na bendi na akapewa jina la Commandant de Bord (CAPTAIN) akiongoza waimbaji wa bendi hiyo bora zaidi kuwahi kutokea Africa.
Mwimbo wake wa kwanza na TP OK Jazz ni “Kebana” wa pili ni “Monzo” 1974 na watatu “Se Lija” 1975. Onja Kebana.
[KEBANA]
Safu yao miaka ya 1970s ilikuwa na Boyibanda Michael (1964), Youlou Mabiala (1966 akarudi mara ya pili 1975 akakutana na JKL), Lola Checain (1967), Sam Mangwana (1972-1975), Wuta Mayi (1974) huyu alikuwa na Josky Continental. Wengine ni Ndombe Opetum “Pepe” (1975), Diatho Lukoki, Djo Mpoyi, Ntessa Daliensti (1977-1986) etc. Sam aliondoka (1975), Boyibanda na Youlou (1977) hii ilimuacha Josky kutawala jukwaa na kuongoza safu ya waimbaji.
Kama Vicky Longomba alikuwa mwimbaji bora wa OK Jazz basi kwangu mimi Mwimbaji bora wa TP OK Jazz ni Josky Kiambukuta, ameimba nyimbo nyingi zaidi kuliko muimbaji yeyote hivyo yeye ni sauti ya TP OK Jazz kama Vicky alivyokuwa sauti ya OK Jazz. Baada ya Vicky kutoka OK Jazz na kuanzisha Orchestre Lovy du Zaire OK Jazz ilijikweza na kubadili jina na kuwa TP OK Jazz.
Josky hakuwa tu mwimbaji bali alikuwa mtungaji bora-nyimbo za hali ya juu na nyingi. Watungaji wa kuu wa bendi walikua Franco, Vicky Longomba, Simaro Lutumba, Josky Kiambukuta (Kundi la kwanza).
Sifa maalum za Josky ni mwanamuziki wa kwanza kuruhusiwa na Franco kutoa Album yake 1983 (Franco Presente Josky Kiambukuta 1983 yenye Alita Tshamala, Mehdi, na nyingine mbili.
Katika project ya “Lisanga ya Banganga” ndio mwimbaji wa pekee kutoka TP OK Jazz aliongozana na Franco (mi solo guitar, au solo ya pili, hupenda kuiita hii solo chombeza) kushirikiana na Tabu Ley (album ya Ngungi). Franco alikwenda na Josky mwimbaji na Matalanza Saxa tu, waliobaki wote ni section Afrisa ya Tabu Ley na Mavatiku Visi Michelino (Ex Afrisa na Ex- OK Jazz) solo guitar. Msikilize Tabu Ley akisema Kiambukuta “pembeni na ngai”. Kolata Pon Pon, Tabu Ley na JKL wakaimba solo kila mmoja kwenye Omona Wapi na kujiitikia wenyewe.
Franco na Michelino Mavatiku Vissi walitoa album nyingine (Benediction 1983) na mwimbaji mkuu akiwa Josky. Kuna nyimbo kama tatu hapo JKL anaimba sauti zote unazo zisikia. Halafu wakatoa album mbili Franco and Josky Kiambukuta du TP OK Jazz (Tout Feu Tout Flamme Vol 1 na Vol 2) wakishirikiana na Michelino kwenye Solo na Franco Mi Solo. Hapa tena kuna nyimbo nyingi ambazo ndani yake sauti zote unazosikia ni za Josky Kiambukuta.
[Point Carre]
Kwa kipekee kabisa range ya sauti ya Josky haijapata kutokea ndani ya TP OK Jazz anaweza akapanda na kushuka kama atakavyo bila kukata punzi na ndio maana kuna hizo rekodi nilizotaja hapo juu ambazo anaimba sauti zote 3-4 peke yake. Kwa kukosa neno la kiufundi nitasema Josky ana imba kwa madaha makubwa kuna muda utafikiri punzi inataka kukata kumbe ni style yake. Ni bora sana kwenye nyimbo za kuimbisha na kupokezana pamoja na kuweka vibwagizo vya sauti. Kubwa kabisa ana haiba ya urafiki. Mwaka huo huo 1983 aliongoza mashambulizi kwenye nyimbo kadha za Lutumba Simaro.
Mafanikio yake ya mwaka 1983 yalikuwa makubwa sana hadi Franco akaona ampige break kupunguza makali na hapo ndio akaibuliwa Madilu System 1983 kwenye kibao “Non”. Madillu alijiunga na TP OK Jazz mwaka 1980. (Ikumbukwe 1974 baada ya Simaro kushusha ngoma ya Mabele Ntotu ambayo ilivuruga charti za DRC Franco alipiga marufuku bendi yake kwa miezi 6 kupiga tungo ambazo hazikuwa zake kuwakumbusha bosi ni nani).
Mwisho wa 1985 baada ya kuhisi kuwa hawapewi heshima yao ipasavyo na bosi wao, Josky Kiambukuta na Ntessa Daliensti (Muzi na Bina Nangai na Respect) walitoka OK Jazz 1986 na huko walikokuwa waliwasha moto-mfano “Le Monde et ses problemes” na “ Ayez Pitie” za Joskyna Selengina ya Ntessa.
Wapenzi wa OK Jazz walipiga kelele hadi 1987 Franco ikabidi awaombe wawili hao kurejea. Ntessa hakurudi bali alifanya Collaborator akitoa album mbili na TP OK Jazz na Josky yeye alirudi na kuendelea kushusha vitu kama “Minzata” na “Kita Mata Bloque”. Madilu alikuwa anamuita jamaa “Kaka” na wawili hawa waliendelea kushirikiana hata baada ya kifo cha Franco ndani na nje ya TP OK Jazz.
Upande wa collabo amepiga nyingi akiwa ndani na nje ya OK Jazz wakati wengine walikuwa wanabanwa au kufukuzwa na Luambo kwa kitu kama hicho. Koffi Olomide kabla ya kuanza Quarter Latin alipiga collabo kali na Josky, tafuta album zake za kwanza Ngounda, Ngobila (1986) utamsikia simba huyu akinguruma.
[Ngobila]
Wengine alipiga collabo nao ni pamoja na Wenge Musica, Zaiko Langa Langa, Victoria Eleyson (concerts), Youlou Mabiala, Madilu system, Malage de Lugendo na Shiko Mawatu, Sam Mangwana, Shiko Mawatu. Koffi Olomide anasema huwezi kutaja waimbaji nguli wa DRC kumi bila kumuweka Josky Kiambukuta kwenye orodha hiyo. Mwaka wa Jana alifanyiwa “Concert” Maalum ya Kusherehekea miaka 69 na wanamuziki wa Bana OK wa Ulaya.
Baada ya kifo cha Franco 1989 yeye alipandishwa hadhi na kuwa Vice President wa TP OK Jazz hadi bendi iliposambaratika. Familia ya Franco ilimtaka Josky awe kiongozi wa TP OK Jazz baadala ya Lutumba Simaro. Kwa heshima aliyokuwa nayo kwa Simaro Josky alikataa majukumu hayo na kama wanamuziki wengine wote wali iacha bendi ya TP OK Jazz na Josky akashauri waite bendi yao mpya “Bana OK” chini ya President Lutumba akisaidiwa na Josky Kiambukuta na Pepe Ndombe Opetum pamoja na Makoso.
Josky aliondoka kwenda Ulaya mwaka 2001 na huko alikuwa akitoa nyimbo chini ya label ya Bana OK, lakinimwaka 2017 alijiunga tena na OK Jazz iliyofufuliwa na kijana wa Luambo bahati mbaya alishikwa na aina ya stroke ikabidi ashughulikie matibabu yake na sasa anapata afueni lakini hajarejea tena jukwaani.
[Double Vie]
Koffi Olomide aliahidi kuwa na usiku wa “Koffi Olomide Chante Josky Kiambukuta” hii inafuatia zile za siku za Koffi kuimba nyimbo za Tabu Ley, Franco na Simaro Lutumba kwa siku tofauti.
Happy Birthday “Le Commandant de Bord” Josky Kiambukuta du Bana OK, TP OK Jazz, Le Orchestre Continental, Le African Fiesta Sukisa.
Soeto Josky et TP OK Jazz