Mfahamu kiongozi wa waasi wa M23

Mfahamu kiongozi wa waasi wa M23

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Kiongozi mkuu wa makundi ya waasi mashariki mwa Kongo Corneille Nangaa, Nangaa ni mfano wa viongozi wengi wa dunia ya tatu.

Nangaa sababu ya yeye kuingia kwenye uasi anasema ni kwamba alipokuwa mkuu wa tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo maarufu kama CENI alishirikiana na mteule wake Rais Joseph Kabila kuchakakachua matokeo ili kumpatia ushindi Felix Tshisekedi lakini baada ya Tshisekedi kushinda alimgeuka waliyoahidiana, madai ambayo Tshisekedi ameyakana vikali

Kiufupi Nangaa ni mzee wa madili.

Dunia ya tatu bado maamuzi ya wananchi yanachezewa mno na magenge ya wahuni wachache wanaobatilisha maamuzi ya wananchi walio wengi na kuwapa ushindi watu wawatakao wao na sio waliochaguliwa na wananchi.

Ndio sababu ya viongozi wengi wasio na sifa kutangazwa washindi huku watu wengi wema kabisa wenye uwezo mkubwa wa kuwa viongozi waadilifu na wenye uwezo mkubwa wakiibiwa ushindi wao

Kwa mwenendo huo nchi nyingi za dunia ya tatu zinaendelea kuwa na utitiri wa viongozi bogus, viongozi mizigo, viongozi incompetent wasio na uwezo wala maarifa ya kusongesha mbele mataifa yao

Kiufupi kinachofanyika dunia ya tatu mara nyingi ni UCHAFUZI sio UCHAGUZI
 
Hilo liko wazi, Baya zaidi ni hilo la yule mwizi mmoja aliyesalitiwa na mwenzake kutumia zile pesa za wizi ku mobilize watu walioibiwa kwenda kumtoa mwenzake madarakani ili akae yeye. Na watu wapo tayari kufa kabisa kwaajili yao.
 
Kiongozi mkuu wa makundi ya waasi mashariki mwa Kongo Corneille Nangaa, Nangaa ni mfano wa viongozi wengi wa dunia ya tatu.

Nangaa sababu ya yeye kuingia kwenye uasi anasema ni kwamba alipokuwa mkuu wa tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo maarufu kama CENI alishirikiana na mteule wake Rais Joseph Kabila kuchakakachua matokeo ili kumpatia ushindi Felix Tshisekedi lakini baada ya Tshisekedi kushinda alimgeuka waliyoahidiana, madai ambayo Tshisekedi ameyakana vikali

Kiufupi Nangaa ni mzee wa madili.

Dunia ya tatu bado maamuzi ya wananchi yanachezewa mno na magenge ya wahuni wachache wanaobatilisha maamuzi ya wananchi walio wengi na kuwapa ushindi watu wawatakao wao na sio waliochaguliwa na wananchi.

Ndio sababu ya viongozi wengi wasio na sifa kutangazwa washindi huku watu wengi wema kabisa wenye uwezo mkubwa wa kuwa viongozi waadilifu na wenye uwezo mkubwa wakiibiwa ushindi wao

Kwa mwenendo huo nchi nyingi za dunia ya tatu zinaendelea kuwa na utitiri wa viongozi bogus, viongozi mizigo, viongozi incompetent wasio na uwezo wala maarifa ya kusongesha mbele mataifa yao

Kiufupi kinachofanyika dunia ya tatu mara nyingi ni UCHAFUZI sio UCHAGUZI
Inatia shaka sana kutegemea mchakachuaji Corneille Nangaa Yobeluo alete mabadiliko ya kweli. Alipaswa kwanza kutubu uhalifu na uchafuzi alioufanya na kumnyima ushindi wa wazi kabisa Martin Fayulu
 
Mimi nina shangazi yupo Sudan UMoja wa mataifa alisema Ajira yake imetokana na hizi VITA na hizi VITA ndo zimempa utajiri

So huwa najua kabisa hao. M23 wapo hapo kimaslahi ya wanasiasa.
 
Back
Top Bottom