Mfahamu kwa picha Prince Rahim Aga Khan mrithi wa nafasi ya Kiongozi Mkuu wa Waislamu wa madhehebu ya washia wa Ismailia.

Mfahamu kwa picha Prince Rahim Aga Khan mrithi wa nafasi ya Kiongozi Mkuu wa Waislamu wa madhehebu ya washia wa Ismailia.

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau hamjamboni nyote?


#Repost @mwananchi_official
——
Mwana Mfalme Rahim Al-Hussaini ameteuliwa kuwa Imam wa 50 wa madhehebu ya Ismailia kufuatia kifo cha baba yake Mtukufu Aga Khan IV, ambaye alifariki dunia jana, Jumanne Februari 4, 2025, jijini Lisbon, Ureno.

Mwana Mfalme Rahim anayekuwa Imamu wa 50 wa madhehebu ya Shia Ismailia, ametangazwa kurithi nafasi hiyo, baada ya kufunguliwa kwa wosia wa marehemu baba yake.

Katika kipindi cha miaka 1,400 ya historia yao, waumini wa Ismailia wameongozwa na Imamu wa kizazi cha urithi. Waismailia wanaishi kwenye zaidi ya nchi 35 na idadi yao inakadiriwa kuwa kati ya milioni 12 hadi 15.

Rahim alizaliwa Oktoba 12, 1971, na ni mtoto wa kwanza wa Mwana Mfalme Karim Aga Khan na mkewe wa kwanza, Binti Mfalme Salimah.
Mwana Mfalme Rahim alipata elimu yake katika Shule ya Phillips Academy Andover na alihitimu mwaka 1995 katika Chuo Kikuu cha Brown na kutunukiwa Shahada ya Sanaa katika Fasihi Linganishi.

Ana watoto wawili Mwana Mfalme Irfan (aliyezaliwa 2015) na Mwana Mfalme Sinan (aliyezaliwa 2017).
Ni msimamizi katika bodi za mashirika mengi ya Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN) na amekuwa akifuatilia kwa karibu kazi ya Taasisi ya Mafunzo ya Ismailia pamoja na taasisi za kijamii za jamii ya Ismailia.

Mwana Mfalme Rahim amejikita katika kusimamia AKDN ili kulinda mazingira na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, akihudumu kama Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira na Tabianchi.

Pia, ameonyesha kujitolea katika kusaidia kazi za AKDN na taasisi za jamii ya Ismailia katika kukabiliana na changamoto za umasikini, elimu, mafunzo na ujasiriamali.

Mwana Mfalme Rahim hukutana mara kwa mara na viongozi wa Serikali, mashirika ya kimataifa, na asasi za kiraia ili kuimarisha mahusiano yao na Imamu wa Ismailia na kuendeleza juhudi za AKDN za kuboresha maisha ya jamii zilizo pembezoni na zilizo hatarini zaidi.


Prince Prince Rahim Aga Khan amezaliwa 12 Octoba 1971 ni mtoto wa pili kati ya Watoto wanne wa marehemu Aga Khan IV.

Amekuwa akiishi Geneva nchini Switzerland.

Ndiye atakuwa mrithi wa nafasi ya Kiongozi Mkuu wa Waislamu wa madhehebu ya washia wa Ismailia


Mamake anaitwa Sarah Frances Croker Poole


Prince Rahim is the second of His Highness the Aga Khan's four children. Based in Geneva, he is Chair of the Executive Committee of the Aga Khan Agency for Microfinance and is a member of the Board of the Fondation de Chantilly in France.

A graduate of Brown University, Rhode Island, USA, with a Bachelor's Degree in Comparative Literature awarded in 1996, Prince Rahim received his secondary education at Phillips Academy, Andover, Massachusetts. After spending some time in the construction sector, in 2006, Prince Rahim completed an executive development programme in management and administration, at the University of Navarra IESE Business School in Barcelona, Spain, before joining the Aga Khan Development Network (AKDN).

Prince Rahim travels regularly to Asia and Africa to oversee microfinance programmes and other projects of the AK
DN.


Prince Rahim married Kendra Irene Spears on 31 August 2013 in Geneva, Switzerland.They have two children: Prince Irfan (b. 11 April 2015)[11] and Prince Sinan (b. 2 January 2017).The couple divorced in February 2022.

In 2019, he bought a house in Unstad in Vestvågøy Municipality, Norway


futureplusbegumpluskendraplussalwaplusspearsplusg75k0oudtfmx.jpg
 
Hivi ndo waanzilishi wa hospital ya aga Khan??

Na mtandao wa The Aga Khan Development Network (AKDN) wenye vyuo vikuu, mahospitali, vitega uchumi duniani kote ikiwemo Tanzania yetu yenye uhusiano wa karibu na Aga Khan mwenyewe kupitia mapenzi ya Babu yake kwa BAKWATA ya zamani EAMWS ....

Soma uzi huu kutoka MAKTABA :
 
Sasa mbona hana sijida?
Kuna waisilamu

Ambao waisilamu wamegawanyika makundi mawili Sunni na Shia.


Ambao Shia nao wamegawanyika kuna Twelver, Ismaili etc Aga Khan ni ismaili, na Shia majority wanaswali Swala 3.

Hao ismail nao wamegawanyika kuna Nizar, Dawood Bohra etc. AGA KHAN ni Nizar

Hao Nizar Ismaili hawaswali kama waisilamu kawaida, wanaenda Jamatini mostly jioni na kurudi nyumbani.
 
Kuna waisilamu

Ambao waisilamu wamegawanyika makundi mawili Sunni na Shia.


Ambao Shia nao wamegawanyika kuna Twelver, Ismaili etc Aga Khan ni ismaili, na Shia majority wanaswali Swala 3.

Hao ismail nao wamegawanyika kuna Nizar, Dawood Bohra etc. AGA KHAN ni Nizar

Hao Nizar Ismaili hawaswali kama waisilamu kawaida, wanaenda Jamatini mostly jioni na kurudi nyumbani.
Safi sanaa wagalatia kama Yoda Azarel Bams waje wajifunze
 
Kuna waisilamu

Ambao waisilamu wamegawanyika makundi mawili Sunni na Shia.


Ambao Shia nao wamegawanyika kuna Twelver, Ismaili etc Aga Khan ni ismaili, na Shia majority wanaswali Swala 3.

Hao ismail nao wamegawanyika kuna Nizar, Dawood Bohra etc. AGA KHAN ni Nizar

Hao Nizar Ismaili hawaswali kama waisilamu kawaida, wanaenda Jamatini mostly jioni na kurudi nyumbani.
Hao Nizar Ismaili wanajitambua hakuna sababu za msingi za kupoteza muda.
 
Hao Nizar Ismaili wanajitambua hakuna sababu za msingi za kupoteza muda.
Technically wenzao ismaili ambao bado ni religious kama Bohra wamefanya makubwa Nchi hii na investment zao zina angalia maisha ya kawaida ya mtu wa Chini.

Ukiangalia Aga Khan ngumu sana kwa Mwananchi wa kawaida ku afford service zake kuanzia shule zake hadi Hospitali, Yupo kibepari zaidi,

Ila Bohra wao wapo kwa Mwananchi wa Chini zaidi na kumuinua masikini ili kesho na yeye awe na kipato kikubwa.

Shule zao bei za kawaida unakuta Ada 1M, si hela ndogo ila kwa quality za Shule zao ambazo almost wanafunzi wote wanapata div one na two ni katika shule bora zaidi nchi hii za bei hio.

Wao ndio wamekamata soko lote la wajasiriamali wanauza kemikali na material mbalimbali ya kutengeneza sabuni, lotion, mabatiki na bidhaa nyingi ambazo wajasiriamali wadogo zinawatoa.

Pia utawakuta wengi kariakoo wakiuza vitu essential kama Stationery za shule, vifaa vya ushonaji, gift shop, vifaa vya keki na vitu vingi vinavyosuport kujiajiri.

So watu ambao hawakumfata Aga Khan ndio wana msaada mkubwa sana Nchi hii, Dini inasaidia kuwa na huruma na kutochaji super profit,
 
Huo uprince ameupataje pataje?
Mbona imekaa kama falme isiyo na ardhi au nchi?

Hapa Tanzania wana balozi wao?
Tufafanulieni sisi maamuma tupate kuelewa.
 
Back
Top Bottom