I am Groot
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,929
- 10,747
Laika, mbwa wa kwanza kufika anga za juu za dunia.
Mbwa huyu ndiye alikuwa kiumbe wa kwanza anayeishi kufika katika nzingo wa dunia, safari hiyo ikifanikishwa na chombo cha anga za juu cha nchini Urusi, kwa kutumia mfano wa satelite ya majiribio ya kisoviet Sputnik 2 mnamo novemba 3, 1957.
Laika alikuwa mbwa mdogo tu wa kg 6 na miaka 2 hivi, mwenye muonekano usiopendeza kutokana na kuwa mixed-breed dog, huku akichangiwa na hasira za karibu. Alikuwa ni mmoja wa mbwa koko pale katika eneo moja nchini Urusi ambao walikusanywa na kupelekwa kwenye programu ya maswala ya anga ya kisoviet baada ya kuokolewa kutoka mtaani. Mbwa jike pekee walionekana kufaa automatic kuliko madume kwa ajili ya majaribio yao.
Laika alipewa mafunzo kwa kujifunza namna ya kukubaliana na kuishi katika sehemu finyu. Pia, walimpa mafunzo makali kwa kumzungusha na kubadili hali ya gravity, namna ya kumudu hali ya kutokuwa na uzito na kukubali kula kwa namna tofauti na alivyozoea.
Kipindi wakati wa maandalizi kabla ya chombo cha Sputnik 2 kuondoka, tukio hilo la kupeleka kiumbe hai outer space ilitangazwa, Laika akawa staa mkubwa wa kimataifa.
Satelite na Abiria wake ghafla ikawa habari ya town kwenye vyombo mbalimbali vya habari na magazeti kote ulimwenguni, huku magazeti ya Urusi wa wakiipa jina la nickname “Muttnik.”
Ilijulikana kabisa Laika asingeweza kupona katika mission ile, Laika alifanikiwa kuishi kwa muda mfupi, kwa masaa 5 baada ya chombo kuruka. Kabla hajafa alionekana kuzidiwa na Joto na panic iliyoletwa na mabadiliko ya kiuzito ndani ya chombo kitu kilichofanya mapigo ya moyo ya Laika kwenda juu ndipo alipopoteza maisha.
Hata hivyo duru za shirika hilo la anga la kisoviet zilieleza kuwa mbwa huyo aliishi kwa muda wa siku 5 angani kabla Oxygen haijamuishia.
Mnamo April 14, 1958 Satelite hiyo iliingia tena katika ozoni ya dunia na kuharibika kabisa.
Hata hivyo, baada ya Laika kushindwa kurudi, bado wanasayansi walichagua mbwa wengine tena wawili waliojulikana kwa jina la Belka & Strelka katika mission iliyofuata, ambayo waliizunguka dunia 1960 na kufanikiwa kurudi duniani wakiwa hai na salama.
::Jina LAIKA lilitokana na neno la kirusi ambalo lilitafsirika kama “bark" au "Bweka" kwa kiswahili. Laika limeingizwa kutumika kwenye majina ya moja ya breed za mbwa huko Russia, ila haihusiani kabisa na mbwa huyu wa angani. Mwaka 2008 kasanamu kadogo cha Laika kalisimikwa katika mji wa Moscow nchini Urusi.