Mfahamu Li lianje [Jet Li] legendary wa muvi anayeteseka na ugonjwa miaka 10

Mockingbird

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2018
Posts
434
Reaction score
1,043
Early this week Nilipata mshituko mkubwa kuona taarifa E-Newz ya muigizaji wa kichina Jet li anavyoteseja na ugonjwa kwa miaka 10.
Tumfahamu jet li ni nani?
Anaitwa Li Lianjie kazaliwa 26/4/1963, anafahamika kama Jet Li
ni Muigizaji,Mtayarishaji wa muvi,Bingwa wa Wushu na Martial Artist.

Kazaliwa Beijing nchini china, kwa sasa ni raia wa Singapore.
Ni kijana mdogo kati ya familia ya wasichana waiwili na wavulana wawili. Baba yake kafariki Li akiwa na Miaka 2.
Li alipokua na miaka 8 ndipo kipaji na uwezo mkubwa wa Wushu ulipogunduliwa wakati wa mashindano ya shule yaliitwa Summer Course. baadae akajiunga na mashindano ya Non sparing wushu Event huko alipata makocha wawili ambao ni Wu bin na Li junfeng, Wu bin ndo alikua anapeleka chakula nyumbani kwa jet li.
Siku moja alipokua bado mtoto alienda kushiriki mashindano ya Chinese National Wushu Team mbele ya Rais Richard Nixon Marekani, Rais Nixon akamwomba Li awe mlinzi wake binafsi (Personal Bodyguard) lakini Li alimjibu "I don't want to protect any individual, when I grow up I want to defend my one billions Chinese Countrymen"
Li ni master wa mapigo mbalimbali kama vile
Changquan,fanzquan,Taijiquan etc.
Baada ya Li kua mshindi wa mashindano mbalimbali nchini China (Bara)hadi Hong Kong (visiwani) Ilikua mwaka 1982 nchini ufilipino ndio alipopata jina la Jet le, Wafilipino waliona jina la Li Lianjie ni gumu kulitamka hivyo wakaona uwezo wa wepesi na uharaka akiwa anapambana wakaufananisha na ndege aina ya Jet hapo ndio jina la jet lilipozaliwa na muvi yake ya kwanza kuicheza wakamwandika Jet Li hapo ndio jina lake likakuaa kuliko la alillo zaliwa nalo Li lianjie.

Muvi yake ya Kwanza kucheza na kumpa jina ulimwengu wa filamu iliku
Shaolin Temple (1,2&3) 1982
One upon a time in China (1,2&3)
Fist of Legend
Fong sai yuk

Mwaka 1998 Li alifanya filamu na Wamarekani inayokwenda kwa jina la Lethal Weapon 4 , alitakiwa kucheza kama jambazi ila akakataa ila wakamwahidi kua atashiriki kwenye filamu nyingine kama starling akakubali. Mwaka 2000 ndipo akacheza kama sterling akishirikiana na mwanamuziki Aaliyah filamu iliitwa Romea Must Die! Filamu iliuza sana. Li aliongea kingereza kidogo sana.

Baadhi ya usiyoyajua kuhusu Li.
Li
alikataa kuicheza muvi ya Crouching Tiger na Hidden Dragon kwasababu alimwahidi Mke wake kua hatacheza muvi yoyote akiwa na mimba nafasi yake ilichukuliwa na Chow yun-fat ilikua mwaka 2000.

Pia alikataa kuigiza kama Seraph katika Muvi ya Matrix kwasababu eti sehemu alizitakiwa acheze hazitumii uwezo alionao wa mapigano, Nafadi yake ilichukuliwa na Collin Chou.
PrayForJetLi.
Jet li is better than Donie Yen & Jackchan.

Alamsiki.
-O'Brian
 
hujatuambia huo ugonjwa unaomsumbua kwa miaka 10 sasa ni ugonjwa gani? na nini hasa chanzo cha ugonjwa huo? wataalam wamesemaje kuhusu tiba ya ugonjwa wake?

naona umetoa tu historia ya jetli na muvi alizocheza/alizotakiwa kucheza...tofauti na kichwa cha habari.
 
Sasa anaumwa lkn unaleta details za movie badala ya tatizo lake?
 
Anasumbuliwa na ugonjwa wa uti wa mgongo,lakini sio serious kivile,
pia jetlee alishakuwa mzee,na ana kipara sikuhizi ukikutana nae unaweza usimjue,
means career yake ndo ishafika mwisho kwani yale madoido na kashikashi hawezi tena,
NOTHING IS PERMANENT
 
Aisee kwel Hilo jina lake la awal llikuwa gumu mi mwenyewe kidogo ulimi niungate
 
Miaka 55 si umri wa kuzeeka kwa huko mambele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…