sembo
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 4,350
- 3,451
20.09.2015.. Taifa Stadium.. Kulikua na mechi ya kukata na shoka kati ya Simba S.C na Kagera Sugar. Japo Mnyama alitawala mechi vya kutosha.. Kulikua kuna "kiumbe" mmoja hivi akiisumbua vya kutosha ngome ya Mnyama.
Ilikua ni Dk. ya 50 tangu mpira uanze huku Kagera Sugar ikiwa nyuma kwa goli 2-0.. Kiumbe huyo mwenye kipaji cha ajabu sana "wonderkid" aliichachafya vya kutosha safu ya ulinzi ya Simba S.C [Great Wall of China] na kutupia moja ya magoli saafi kabisa, kuwahi kushuhudiwa katika uwanja huo.
Huyu si mwingine bali ni zao toka Simba B, 'Mtalaamu' Mubarak Yusuph "Boban".. anayewatumikia wakata miwa kwa mkopo wa mda mrefu akitokea Simba S.C.
Mubarak ni miongoni mwa wahitimu wa mwaka huu toka chuo chetu [Simba B].. Baadhi ya wahitimu wenzake ni Boniphace Maganga na Said Abdallah ambao wapo kikosi cha wakubwa cha Simba S.C.
Wiki iliyopita nikiwa mkoani Tabora, nilibahatika kushudia mazoezi ya Timu ya Kagera Sugar katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi. Hapo ndipo sikuamini kwa mara nyingine tena, kutokana na kile nilichokishudia machoni mwangu toka kwa huyu kijana Mubarak.
Mubarak amebarikiwa kipaji cha aina yake, kwani akiwa bado kinda tayari ana uwezo mkubwa wa kufunga kadiri anavyojisikia na hii ni kutokana na uwezo binafsi na nguvu alizojaliwa.. Pia zile zinazoitwa pasi rula hapa ndo nyumbani.
Nadiriki kusema, Mubarak Yusuph ni kopi ya Gwiji, Zvonimir Boban toka Crotia.. kwani ana kila kitu.. unachokifahamu toka kwa Boban.
Kocha Mkuu wa wakata miwa, Mbwana Makata [kocha bora wa VPL, msimu wa 2014/15] mwanzoni mwa msimu huu alinena.. namnukuu...
"Kwa ujumla nimeridhika na kiwango cha Boban na kama ataendelea hivi, ni dhahiri atakua na mchango mkubwa kwenye timu yangu".
Anaendelea... "Kama unavyojua mashabiki walikua na mashaka baada ya wachezaji muhimu, Rashid Mandawa na Atupele Green kuondoka, nadhani hilo sasa watalisahau".. Nami naungana nae kwa 100.05℅.
Japo huu ndo msimu wake wa kwanza katika VPL.. hadi hivi sasa Mubarak kashikana koo na kina Msuva, Busungu, Mandawa, Allan Wanga, Vincent Barnabas n.k katika kutupia kambani... wote wakiwa na goli 1.
Nakutakia kila la heri Mubarak Yusuph "Boban".. Naimani msimu ujao utarudi nyumbani ukiwa strong zaidi.. Na utaendelea kutunyanyua vitini kama kawaida yako.
Mungu Ibariki Simba B.. Mungu Ibariki S.C.