Mfahamu Mfalme Leopard aliyetawala Congo na maasi aliyowafanyia Waafrika

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Leopold II alitawala Congo na ilijulikana kama nchi ilikuwa mali yake binafsi, miaka ya 1835. Tofauti na ilivyokuwa South Afrika kama koloni la Uingereza Congo ilikuwa nchi huru chini ya Mfalime Leopard II




Leopold alizaliwa katika familia ya kifalme mwaka 1835, ujana wake ulikuwa wa kawaida katika makuzi ya kifalme, alitumia muda wake mwingi kujifunza kuwinda, kulenga shabaha, alijiunga na jeshi na alimuoa mtoto wa mfalme wa Austria lakini hakuna aliyetegemea kua atakuja kuwa muuaji wa kushindana na Hitler.


Leopold II aliapishwa kuwa mfalme mwaka 1865 na alitawala Ubelgiji, ndoto yake kubwa ikiwa kuiona Ubelgiji ikiwa na koloni nje ya Ulaya kama ilivyokuwa kwa mataifa makubwa kama Uingereza, Ufaransa, Hispania na Ureno.

Jicho lake la kwanza lilikuwa kuichukua Ufilipino wakati huo likiwa koloni la Hispania. Alitengeneza dili na Malkia Isabella, lakini kabla ya makubaliano kufikia mwisho, malikia Isabella alipinduliwa. Leopard alianza kuangaza macho katika bara la Afrika.

Mwaka 1878, Henry Stanley inasadikika alikutana na Dr. Livingstone katikati ya msitu wa mvua wa Kongo. Magazeti yaliandika habari hii ya kuwapongeza mashujaa hawa wawili kwa kugundua msitu wa Kongo lakini hakuna aliyeuliza wawili hawa walifuata nini kule.

Miaka michache kabla ya mkutano wa Henry Stanley na Dr. Livingston, Leopold II alianzisha African Society iliyoshughulika kuchunguza bara la Afrika na yeye akiwa mfadhili mkuu. Mfalme alipeleka zawadi nyingi kwa raia wa Kongo ikiwemo nguo na magari.

Mfalme Leopold II alifanikiwa kushawishi Congress iliyofanyika 1885 Berlin kuwa Kongo ni nchi huru. Utawala wa Leopold II ulikuwa wa ki dikteta na wa kutisha. Aliua maelfu bila kujali mradi walikwenda kuchimba dhahabu, kuwinda tembo ili apate meno. Wananchi walilimishwa mashamba makubwa ya mpira.


Vijana walilazimishwa kwenda kuvuna raba, aliyeleta kiwango kidogo cha raba alikatwa mkono kama huyo kijana kwenye picha,

Udhalimu uliyofanywa katika nchi huru ya Kongo ulikuwa mkubwa kiasi cha kuwapa hofu nchi nyingine za Ulaya zilizokuwa na makoloni Afrika.



Huyu baba aliitwa Nsala, hapa anaangalia viganja na miguu ya binti yake wa miaka mitano aliyekatwa kama adhabu ya yeye kutokwenda kazini.



Adhabu ya mwanaume ambae hakwenda kazini.
 
Picha zinatisha
Kongo ilikuwa mzalishaji mkubwa wa rubber duniani. Watoto na vijana walipewa vikapu asubuhi kwenda kuvuna rabber iwe mvua iwe jua.
 


Hakuna tofauti yoyote na unyama walioufanya Waingereza, Wafaransa, Wajerumani au sijui Wareno hapa Afrika, tofauti ni kwamba hiyo iko documented tu!
 
Hakuna tofauti yoyote na unyama walioufanya Waingereza, Wafaransa, Wajerumani au sijui Wareno hapa Afrika, tofauti ni kwamba hiyo iko documented tu!
Kama unyama aliotendewa Lisu, SANDARUSI na MKIRU (by Zito Kabwe, Bungeni..380??)
 
His name was Leopold not Leopard
 
Ww jamaaa unawaza kutumia makalio au kichwa maaana hujui ulisemalo
Makalio anatumia mama yako kufikir, Ukinitukana nitakutukana bila kujali lolote! Jibu hoja kwani lazima utukane. Mkiru haipo? Issuwe ya Lisu haipo? Jibu hoja
 
Wacongo wamejazana Ubelgiji,siamini Kama wanaishi kwa amani ndani ya nchi iliyowatendea unyama namna hii,nakumbuka siku moja nilikuwa pale Gare du midi mara nikamsikia mzungu alcoholic anasema Wabelgiji ni wezi waliibia Congo Zaire madini na kuiacha Congo ikiwa na matatizo mpaka leo.Yule mzungu alikuwa anasema ukweli mtupu.Brusels kuna hadi mtaa unaitwa Matonge pale ni Wacongo wamejaa dah kumbe ni ndani ya nchi iliyowanyanyasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…