Ben Zen Tarot
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,298
- 7,612
MICHAEL GRZIMEK Mjerumani mtengeneza filamu za wanyama aliekufa kwa kuanguka na ndege Ngorongoro kreta baada ya ndege yake kugongana na ndege wa porini aina ya tai(vulture). Michael Grzimek alizaliwa 12 April 1934 Berlin Ujerumani,alikuwa mtoto wa pili wa Bernhard Grzimek na Hildegard Plüfer.
Michael alipofikisha miaka 16 alisaidiana na baba yake kwenye utafiti waliokwenda kuufanya Ivory cost.Mafanikio yalianza kuonekana baada ya baba yake kuandika kitabu kinachoitwa keine Platz für wilde Tiere(No room for wild animal)maana yake hakuna chumba kwa mnyama pori, kilichokuwa kinaelezea Safari Yao ya utafiti walioufanya Congo mwaka 1954, Michael alimwambia baba yake watengeneze filamu kutokana na kitabu hicho.
Wakatengeneza filamu ambayo ilipata tuzo mbili,tuzo ya kwanza Ni ya Filamu Bora kutazamwa na ya pili Ni tuzo ya Filamu ya kimataifa mwaka 1956 kwenye tamasha la kimataifa la filamu Berlin,na kuuza nakala ya Filamu kwa nchi 63.Michael akapanga Safari ya kuja Tanganyika ili kurekodi filamu Serengeti, akanunua ndege ya injini moja Aina ya Dornier do 27 akaipaka rangi ya pundamilia.
Akaanza kuruka na ndege kuzunguka Serengeti akiwa anarekodi filamu aliyoipa jina la (Serengeti shall not die)maana yake Serengeti haiwezi kufa. Tarehe 10 January 1959 aliruka na ndege yake kuendelea kurekodi filamu hiyo bahati mbaya aligongana na ndege wa porini Aina ya tai(vulture)na ndege kupoteza muelekeo na kuanguka chini na kusababisha kifo chake.
Alizikwa siku hiyohiyo juu ya kreta ya Ngorongoro na kaburi lake likajengwa Kama piramidi ndogo ya mawe. Baada ya Michael kufariki baba yake alimalizia kurekodi filamu ya Serengeti shall not die, na kufanikiwa kuchukua tuzo ya Filamu bora ya wanyama mwaka 1959, ikawa ndio filamu ya kwanza Ujerumani kupata tuzo hiyo na akaandika na kitabu ambacho alikitafasili lugha 23 na kuuza mamilion ya nakala.
Baba yake michael alikufa 1987 akiwa Ujerumani, na kuchomwa moto majivu yake yakaletwa kuzikwa alipozikwa mtoto wake juu pembezoni mwa kreta ya Ngorongoro Tanzania.