Mfahamu mtu mfupi zaidi duniani anayepiga hela ndefu huko nchini Marekani

Joined
Sep 11, 2014
Posts
34
Reaction score
23
Unaweza kuwa mfupi kiasi cha kukufanya utamani kuongezeka, lakini ukiwaona wenzako wanavyopeta nalo basi utagundua unapaswa kumshukuru Mungu kwa umbo lolote ulilopewa.
Jyoti Amge, mwenye umri wa miaka 21, ndiye mwanamke mwenye kimo kifupi zaidi duniani akiwa na urefu wa inches 24 (sawa na urefu wa rula mbili za sentimita 32).

Jyoti ambaye ni mkazi wa Napur, India, aliingia rasmi katika kitabu cha Guinness mwaka 2011 kama mwanamke mfupi zaidi duniani aliye hai na tayari ameshapata deals kubwa kwa kimo chake.
Amewahi kushiriki katika makala maalum ya Body Shock: Two Foot High Teen na August 13, na mwaka huu alipata deal ya kuigiza katika ‘American Horror Story: Freak Show’.

Mwanamke huyo ambaye kimo chake kinatajwa kuwa kimetokana na tatizo la kutokua kawaida ‘achondroplasia’ anaendelea kupiga deals kubwa na amegeuka kuwa lulu kwa muonekano huo wa kipekee.

Jyoti akiwa amebebwa
 
Du mungu mkubwa kweli kila kitu na sababu yake usichukie allah alichokupa
 
Huyo Tall sana kuna mmoja nimemuona Dodoma (one way) ni mfupi kuliko huyo na anaonekana ana zaidi ya 40yrs. Hatangazwi kutokana na Media zetu tu. Sikubahatika kuchukua picha kwani nilihofu naweza kumkwaza hata ningemuomba.
 
Kabisa mkuu, yule wa DODOMA ana watoto 2 kwa sasa, mara nyingi utamkuta mnadani pia, naunga mkono hoja yako kuwa ni vile media za TANZANIA hazijafanya kazi ya kutosha kuangalia watu kama hao na namna wanavyoweza kutangazwa vema.
 
Bora umenisaidia kwa hilo.
 
Ila kazuriii,hadi nimekapenda jamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…