Raj kapool
JF-Expert Member
- Jun 29, 2018
- 1,352
- 2,160
Naam ni Nuri Sahin alikuwa playmaker Mwenye kipawa cha Aina yake Ila alinyimwa bahati mwishoe kwenye career yake akaandamwa na majeraha.
Mnamo 1989 ndio Alizaliwa Nuri Şahin huku wazazi wake wakiwa na asili ya Kituruki Japo waliishi Germany katika Jimbo la Lüdenscheid, takriban kilomita 40 nje ya Dortmund.
Alijiunga na BVB kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 12 ilikua 2001, hiyo ndio ilikua club ya Ndoto yake Ila Fernando Redondo na Zinedine Zidane tokea Madrid hao ndio Wachezaji waliokua wakimvutia.
Mwenyewe Aliwahi kusema "katika usiku wa ulaya 2002 Nakumbuka jezi nzuri nyeupe ambazo Madrid ilivaa usiku huo, Zilikuwa za kushangaza, walicheza mpira wa ajabu sana.
Wakati fulani katika mechi hiyo kipindi cha pili nakumbuka nilikua nikifikiria kua Sawa nitachezea Dortmund, Lakini hata iweje nitacheza pia Real Madrid".
Msimu 2010/11 Borussia Dortmund walitwaa ubingwa kibabe Sana wakiwa na akina Mats Hummels, Mario Götze, Shinji Kagawa, Robert Lewandowski.
Pia alikuepo Mkurugenzi wa sasa wa michezo wa Dortmud bwana Sebastian Kehl alikuwa nahodha na hata kocha msaidizi wa sasa bwana Sven Bender alicheza pamoja na Sahin katika safu ya kiungo.
Sahin akiwa kijana mdogo Aliekua mhimili wa Klopp na kuisababishia dortmud mafanikio makubwa, klopp alimuahidi Sahin kuwa atakuwa rafiki yake wa maisha.
Akiwa Bundasliga alivunja rekodi mbili na kuzishikilia kwa miaka mingi, mpaka pale bwana mdogo Youssoufa Moukoko alipokuja kuzivunja rekodi zote mbili.
Rekodi Ya Kwanza Şahin Alikua mchezaji mwenye umri mdogo zaidi katika ligi hiyo kuccheza mechi ya kwanza akiwa na umri mdogo.
Şahin akiwa na miaka 16, miezi 11 na siku moja, alicheza mechi yake ya Kwanza dakika zote 90 katika sare ya 2-2 dhidi ya Wolfsburg mnamo Agosti 2005,
Rekodi Ya Pili, Sahin alikua mfungaji wa bao angali mdogo zaidi katika Bundasliga.
Akiwa na umri wa miaka 17 na siku 82 alifunga katika ushindi dhidi ya Nuremberg mnamo Novemba mwaka huo huo.
Mwamba Baada ya msimu wa 2010-11 kujitengenezea jina katika timu aipendsyo Dortmud, msimu uliofata aliondoka kama shujaa na kujiunga na Real Madrid timu nyingine ya Ndoto zake.
Akiwa huko madrid Majeraha yalimuandama na mipango haikwenda kama alivyopanga,
Klopp rafiki yake wa faida alimrejesha Dortmund baada ya kucheza kwa mkopo Liverpool.
Sahin aliwahi kusema hivi kuhusu Klopp "Hakuna shaka kuhusu ufundishaji wake - ni mzuri sana,"
Şahin aliiambia Goal mnamo Mei 2021. "Lakini ninachopenda zaidi kwake ni kwamba yeye ni binadamu, Anakugusa kwa kiwango cha kibinadamu ... Hiki ndicho nilichopenda juu yake na kile nilichojifunza juu yake".
Şahin aliendelea "Ikiwa unataka kuwa kocha mzuri kwa muda mrefu zaidi, lazima uwe mtu mzuri pia, kwa sababu wachezaji ni watu pia.
Huwezi kusema kwao uwongo, Jürgen hasemi uwongo.
Yeye yupo vile alivyo, na hii ni sababu moja ya kwa nini amefanikiwa sana". Şahin alimaliza.
Playmaker huyu kutokana na Majeraha aliishia Kucheza michezo 274 ndani ya Dortmud na kufunga goli 26.
Aliwaa Bundasliga 2011 na 2017 ndio mara ya mwisho Kuitumikia Dortmud alishinda Kombe la DFB, kisha akajiunga Kwa miaka miwili pale Werder Bremen.
Mwishoe Aliondoka Germany na kwenda Ardhi ya kwao Uturuki Kunako club ya Antalyaspor mnamo Agosti 2020 na akamaliza maisha yake ya uchezaji na kuwa meneja wa timu hiyo ya Uturuki mnamo Oktoba 2021.
Katika siku zake za mwisho kama mchezaji, kiu ya Şahin ilikua ni kupata maarifa, kiu Hii ilimfanya ajiandikishe katika chuo kikuu maarufu cha Harvard Amerika mnamo 2018.
Mara nyingi alizungumza kuhusu hamu yake ya kujiendeleza zaidi kuja kua kocha bora, alisoma kozi ya usimamizi na biashara katika chuo hicho.
Kila la kheri Nuri Şahin, Nuru iliyowaka ukiwa kinda kisha kufifia na sasa imewaka ukiwa mwalimu wa Borussia Dortmund.