MFAHAMU MWANAMICHEZO WA KIITALIANO ALESSANDRO DEL PIERO

MFAHAMU MWANAMICHEZO WA KIITALIANO ALESSANDRO DEL PIERO

Joined
Jun 25, 2024
Posts
6
Reaction score
6
Anaandika Idd Rashid ( Iddmastory).

Alessandro Del Piero alizaliwa Novemba 9, 1974 huko nchini Italia katika familia ambayo baba yake alikuwa ni fundi umeme na mama yake akiwa ni mama wa nyumbani asiye na kazi yoyote.

Maisha yake ya soka aliyaanza kama mlinda mlango ambapo alikuwa akimfurahisha sana mama yake kwani ilikuwa ni ngumu kwa yeye kupata majeraha na hata kuchoka sana pindi awapo golini. Alidumu katika eneo hilo kwa muda mchache sana hadi pale ambapo kaka yake alimshauri kucheza eneo la mbele kama mfungaji kutokana na namna ambavyo alikuwa hatari zaidi eneo hilo kuliko awapo langoni.

Mwaka 1981 alijiunga na klabu ya San van demiano ambapo alidumu kwa miaka nane hadi 1988 ambapo aliondoka klabuni hapo na kujiunga na klabu ya Padova ambayo aliichezea hadi mwaka 1993 ambapo alicheza michezo 14 na kufunga goli moja pekee.

Mwaka 1993 ulikuwa ni mwaka wa kukumbukwa kwa Alessandro del Piero kwani alijiunga na klabu ya Juventus ambayo aliichezea kwa misimu 19 mfululizo. Akiwa hapo alipewa jina la kiitaliano la "Fantasista" kutokana na namna ambavyo alikuwa amebarikiwa ubunifu na uwezo mkubwa wa kufunga magoli.

Juventus ilikuwa ni klabu aliyocheza kwa mafanikio makubwa sana ambapo miongoni mwa mafanikio hayo ilikuwa ni pamoja na;

🥇Mchezaji bora wa ligi ya Italia serie A ×2.

⚽Mfungaji bora wa ligi kuu ya Italia 2007/2008 akimaliza na magoli 21.

⚽Mfungaji bora wa UEFA champions league 1997 akimaliza na magoli 10.

⚽Mfungaji bora Serie B 2006/2007 akimaliza na magoli 20 ( msimu ambao Juventus ilishushwa daraja).

Akiwa na timu ya taifa ya Italia amecheza michezo 91 na kufunga magoli 27 ambayo yanamfanya ashike nafasi ya nne kwa wafungaji bora wa muda wote wa timu hiyo ya taifa. Akiwa na jezi ya Italia amefanikiwa kupata mafanikio kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na;

🏆Kombe la dunia mwaka 2006.
🏆Mshindi wa pili Euro mwaka 2000.

Katika maisha yake yote ya soka Alessandro Del Piero amefanikiwa kufunga magoli 346 yanayomfanya ashike nafasi ya pili kwa wafungaji bora wa muda wote wa ligi ya Italia kwani orodha inaongozwa na Silivio Piola mwenye mabao 390.

Nje na maisha ya soka Alessandro del Piero ni mtu anayejitoa sana kusaidia watu kwani mwaka 1998 alitoa zaidi ya 5.2 lire kusaidia watoto waliotelekezwa mtaani pamoja na waathirika wa ugonjwa wa UKIMWI.
 

Attachments

  • 800px-Alessandro_Del_Piero_2008_cropped.jpg
    800px-Alessandro_Del_Piero_2008_cropped.jpg
    199.6 KB · Views: 7
Back
Top Bottom