Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Baada ya kuhangaika kwa miaka mingi sana leo nimejaaliwa kupata picha ya Mzee bin Sudi na picha hii kanipatia mjukuu wake Bi. Subira Mohamed Sudi.
Rafiki yangu na mzungumzaji wangu marehemu Athumani Kassanda (amefariki kiasi cha miezi kama minne iliyopita) siku moja katika mazungumzo yetu ya kawaida nilimuuliza wapi naweza kupata picha ya Mzee bin Sudi.
Sheikh Kassanda alikuwa na taarifa nyingi sana za wazee wa Kimanyema na mama yake Bi. Khadija bint Jaffar alikuwa mmoja wa akina mama katika tawi la TANU lilioanzishwa na Ali Masham.
Historia ya Ali Mshama naamini sasa ni maarufu kwa wasomaji wangu. Sheikh Kassanda akaniuliza kama namfahamu Shukuru Sudi.
Nilimwambia sijamuona miaka mingi na kwa miezi minne ikawa nahangaika kumtafuta Shukuru na leo nikapata simu yake kutoka kwa shoga yake Bi. Sikudhani Kassim ambae kwangu mimi ni shangazi yangu lau kama umri wetu unalingana.
Shukuru alishangaa sana nilipojitambulisha akaniambia mara ya mwisho mimi na yeye kuonana ilikuwa England. Nilifurahi kwa Shukuru kutumia hili neno, ‘’England.’’
Hakika mara ya mwisho mimi na shukuru kuonana ilikuwa Finsbury Park, London mwaka wa 1991.
Wakati huo sote tulikuwa vijana.
Nikamuomba Bi. Shukuru picha ya babu yake na tukafanya mazungumzo kidogo kuhusu babu yake huyu.
Bi. Shukuru akaniahidi kunipa picha nyingine na akaniambia kuwa kuna picha maarufu ya babu yake ilitoka katika gazeti magazeti ya chama Uhuru na Mzalendo.
Picha hii inamuonyesha Mzee bin Sudi akisoma hotuba mbele ya Mwalimu Nyerere na mgeni wake Raisi Jaffar Nimeiri wa Sudan wakiwa ya ofisi ya TANU mwaka wa 1972.
In Shaa Allah picha hii ikipatikana nitaiweka hapa kwa faida yetu sote. Turudi kwa babu yake Bi. Shukuru Mzee bin Sudi.
Hiyo ofisi ya TANU ambayo Mzee bin Sudi alisimama kusoma risala ilikuwa ofisi ya African Association (AA) ambayo yeye akiwa Rais wa AA alishiriki ujenzi wake katika ya mwaka wa 1929 – 1933 na ilifunguliwa na Gavana Donald Cameron mwaka wa 1933.
Picha ya sherehe hiyo ya ufunguzi ipo na bila shaka Mzee bin Sudi alikuwapo katika sherehe hii.
Katika picha hii yuko Gavana na pia Kleist Sykes aliyekuwa Katibu wa AA.
Ofisi hii ya AA ndiyo ikaja kuwa ofisi ya TAA pale mwaka wa 1948 AA ilipobadili jina lake na kuwa TAA.
Hii ndiyo nyumba ambayo TANU iliundwa mwaka wa 1954.
Bila shaka kwa Mzee bin Sudi kusimama mbele ya Nyerere na Nimeiri wakiwa katika ofisi ile ya AA ambayo yeye na wenzake walijenga zaidi ya miaka 40 iliyopita hii ni historia ya pekee.
Lakini nani katika wale wote waliokuwapo pale walikuwa wanaijua historia hii?
Mwaka wa 1933 katika uongozi wa TAA Mzee bin Sudi akiwa Rais na Kleist Sykes Katibu palitokea ugomvi baina ya Kleist Sykes na Erika Fiah.
Erika Fiah ndiyo Mwafrika wa kwanza kuwa na gazeti lake ‘’Kwetu,’’ na ingawa gazeti hili lilikuwa ndiyo sauti ya Waafrika wa Tanganyika lakini mara kwa mara Fiah akituia gazeti hili kumshambulia ‘’Mzulu,’’ Kleist Sykes.
Ugomvi huu ukafikia mahali Kleist akajitoa katika uongozi wa AA na nafasi yake ikashikiliwa na Erika Fiah. AA ikawa inadorora kwa kumkosa Kleist.
Mzee Bin Sudi akamwandikia barua Kleist barua ambayo aliianza kwa ‘’Bismillah Rahaman Rahim.’’
Sikutegemea kuona barua ya AA inatangulizwa na maneno hayo matukufu.
Hii ilinifanya nitake angalau kuona picha ya huyu Mzee bin Sudi alikuwa anafananaje.
Barua hii ni katika nyaraka za Sykes ambazo mimi imeniathiri sana si tu kwa kwa kuanza kwa Jina la Allah bali kwa yale maudhui ndani ya barua ile.
Mzee bin Sudi katika barua ile ya mwaka wa 1933 alimkumbusha Kleist madhumuni yao ya kuikomboa Tanganyika.
Mzee bin Sudi akamwambia Kleist azma yao itafikaje tamati kwa mafanikio ikiwa itakuwaje yeye anajiweka pembeni?
Ifahamike kuwa Mzee bin Sudi alikuwa Rais muaisi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Kleist katika barua ya majibu alikiri kuwa kafanya kosa kujiweka pembeni na akamwandikia Mzee bin Sudi maneno haya:
‘’Tupambane kwa nguvu zetu zote kuelekea njia ya ustaarabu kama vile watu wa makabila mengine wanavyofanya. Haidhuru kitu ikiwa hatukamilishi kila kitu.
Wale watakaokuja baada yetu watakamilisha yatakayobakia.’’
Kleist hakuiona Tanganyika huru kwani alifariki mwaka wa 1949 lakini Mzee bin Sudi aliishi na kuiona Tanganyika huru.
Mzee bin Sudi akasimama miezi michache kabla ya kifo chake mwaka wa 1972 kusoma risala mbele ya Nyerere na mgeni wake Jaffar Nimeiri akiwa analiangalia jengo la kupendeza la ofisi ya TANU ambalo chanzo chake ilikuwa ile nyumba yao waliyojenga kwa miti, udongo, chokaa, mawe ya kutomea na kuezekwa na madebe.
Picha hiyo ni Mzee bin Sudi akiwa na wakeze watatu na wajukuu zake akiwa shambani kwake Kwame Mbagala miaka ya mwanzoni 1960s. Huyo aliyekunja mikono ni Shukuru.
Picha ya pili ufunguzi wa ofisi ya African Association mwaka wa 1933. Picha ya tatu ni Erika Fiah.