Mfahamu Mzee Jumbe Muhammad Tambaza

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Alizaliwa January 1891 na kufariki 1978.

Ni miongoni mwa Wazee wa mwanzo, waliompokea, Mwalimu Nyerere kutoka Butiama, alipokuja Jijini Dar es Salaam.

Alimuunga mkono ktk harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika, miaka ya 1950s

Neno, ''Tambaza,'' limetokana na ''Kutambaa,'' au ''Kusambaa,'' eneo kubwa. Diwan Tambaza na nduguze walikuwa watawala wa sehemu mbalimbali za hapa Mzizima siku za nyuma kabla ya Waarabu, Wajerumani na Waingereza kufika.

Nduguze wengine ni..

Diwan Uweje, Diwan Uzasana, Diwani Mwenye-Kuuchimba na Diwan Mwinyi Ndugumbi.

Diwani Mwenye-Kuuchimba, yeye alikuwa akitawala maeneo ya Mtoni Kijichi na Mbagala.

Ukoo wa Diwan Tambaza Zarara Bin Mwinyi-Kitembe ndio waliokuwa wenyeji wa maeneo ya katikati ya Jiji wakati huo.

Eneo la Upanga, kuanzia Daraja la Selender hadi Ikulu ya Magogoni, na kutoka Aga Khan Hospital, Ocean Road..

Hospital, Kivukoni Front (makaburi ya Nduguze yapo pale Wizara ya Utumishi, Magogoni) kwenda Mnara wa Saa pale Uhuru Street.

Eneo la Majengo la Barabara ya Bibi Titi, kwenda Kisutu hadi Kariakoo, liliitwa Tindwa, na ndipo Mji ulipokuwa.

Jina la Mzizima

Eneo la Magogoni hadi Salenda lilijulikana kama Mzizima kutokana na utulivu wake pamoja na wanyama wakali waliokuwepo enzi hizo.

Ikawa kila aliyepita eneo hilo lazima mwili wake uzizime.

Auza Eneo kwa Sultan

Miaka ya 1860s, alimega kuanzia Salenda hadi Magogoni akamuuzia Sultan Majid wa Zanzibar, ambaye alijenga majengo ya Chuo Kikuu

cha Kiislamu, Daru Salaam (hivi sasa Ikulu) na hostel zake, ambazo sasa ni Hospital ya..

Saratani ya Ocean Road.

Kusanyiko la eneo lake la Tindwa, alilouza na la Mzizima alilogawa, ukichanganya na miji ya Kunduchi na Mbwa Maji, ndio yaliyounda Jiji la Dar Es Salaam, jina lililotokana na Daru Salaam.

Wakoloni Watwaa Maeneo

Wakoloni walipokuja, waliipenda madhari ya Upanga.

Wakaona Weusi hawastaili kuishi pale, kina Tambaza wakaamriwa wawapishe Wahindi (daraja la 2).

Hii ni baada ya wao Wazungu(Daraja la 1) kuchukua OysterBay (sasa Masaki)

Makaburi ya Tambaza

Wakolonii hawakutenga sehemu ya kuzikia watu weusi, makaburi ya Kisutu yalikuwa ni ya watu wenye asili ya Kiarabu.

Mwafrika alipelekwe nje ya mji, Kunduchi, Mbweni, Msasani, Bagamoyo na Mwanalumango.

Kuondoa adha hiyo, Mzee Tambaza...

alitoa bure sehemu ya eneo lake litumike kuzikia Waafrika.

Jumbe Tambaza aliwashawishi binamu zake, Mwinyimkuu Mshindo na Diwan Mwinyi Ndungumbi, na wao wakatoa sehemu watu waweze kuzikana.

Maeneo ya Mwinyimkuu, Magomeni Mapipa na Ndugumbi, Magomeni..

Makuti, makaburi ambayo mpaka sasa yanazikia watu wote.

Ziara ya Binti Mfalme
Muhimbili tunayoiona, ilijengwa mwaka 1956, kwa heshima ya Binti Mfalme Margareth II, aliyekuwa na ziara ya kutembelea makoloni, ilitengenezwa,ili aje kuifungua rasmi.

Iliyokuwepo kwa ajili ya watu Weusi ilikuwa ni kama Zahanati tu, jirani na Kituo cha Kati, cha Polisi (Central Police Station) katikati ya Jiji, ikiitwa Sewa Haji Haji Hospital, iliyojengwa na mfadhili kusaidia jamii maskini.

Sewa Haji alikuwa mkazi wa Bagamoyo mwenye asili ya Kibulushi kutoka Persia.

Baada ya kujengwa hospitali ya Muhimbili, jengo moja katika yale matatu makuu, likaitwa Sewa Haji, kama kumbukumbu yake.

Harakati zake ktk kudai Uhuru

Kama niliposema Mwanzo, ktk Wazee waliompokea Mwalimu Mjini, naye ni mmoja wapo.

Alimuita Mwalimu (hapo, Mwalimu Kijana tu) nyumbani kwake, akiwa na Wazee wengine, wamsomea Dua, na kumfanyia tambiko, mabaya yasimpate.

Wakamng'arisha nyota, tayari kwa mapambano ya kudai Uhuru.


Kwenye TANU

Wakati TANU inafanya mkutano wake wa kwanza, pale Arnatoglo, walialikwa Wajumbe 20 tu, akiwemo Mzee Tambaza.

Inasemekana, ilipotokea kutokuelewa kati ya Zuberi Mtemvu..

na Nyerere, Mzee Tambaza alikuwa upande wa Mwalimu.

Kutokana na uaminifu usiotetereka kwa chama, Mzee Jumbe Tambaza na Mwinjuma Mwinyikambi walikuwa na Permanent Seats, kama Wajumbe wa Kamati Kuu, kadhalika Baraza la Wazee.

Mzee Tambaza na Serikali Waburuzana Mahakamani

Mwaka 1950 Mzee Tambaza aliingia ktk mgogoro na Serikali, ilipokuwa inajengwa upya barabara ya Umoja wa Mataifa (UN Road), kutoka Salenda, kuelekea Fire.

Iliamuliwa, baadhi ya..

makaburi yaondolewe, kunyoosha barabara, Mzee Tambaza akagoma, akaenda Mahakamani kufungua "Landmark Case", akashinda.

Ndipo faster akajenga ule Msikiti wa Tambaza, kulinda lile eneo.

Ukitokea Fire, baada ya kupta Swiss Tower, utaona barabara ina kona

Katika Kuthamini Mchango Wake

Iliyokuwa Shule ya Kihindi, enzi za ukoloni, Aga Khan Boys, ikabadilishwa jina, nakuitwa Tambaza Secondary School na Ile Muhimbili Primary, ilikuwa ikiitwa

Aga Khan Girls.

Shule hizi za Aga Khan walikuwa wakisoma Watoto wa Kihindi Tu.

Huyo Ndio Mzee Tambaza

#Gudgudinformer

๐Ÿ™๐ŸฟThank You๐Ÿ™๐Ÿฟ
 
Ahsante kwa historia nzuri,endelea mkuu!
 
Sijaona jina hata moja la mgalatia katika watu wote wenye historia na hii nchi na hasa walioupambania mji huo wa daressalaam, cha ajabu wagalatia wana wadharau waislam na wazaramo wakti ndio born town.
 
Kuna hotuba moja Nyerere anahadithia jinsi alivyorushwa shimo katika matambiko na Jumbe Tambaza, huku Jumbe Tambaza akisema Gavana Twining shwaini tu.

Nyerere na Ukatoliki wake alikuwa anaheshimu sana mambo ya mila.

Kuanzia hapo Gavana akawa hawezi kumwambia kitu Nyerere.

Mzee Pambe alikuwa anaimba wimbo wake mmoja pake makaburini. Akikumbuka siku za zamani.

"Jumbe Tambaza mfano, mtu wa watu.
Akiwa na rupia tano, atagawa tatu."
 
Historia Nzuri. Ukisoma Sheria ya Ardhi, katika Land History in Tanzania, basi huyu Mzee Muhamed Tambaza utakutana na jina lake humo. Namna ambavyo wakoloni walipata shida kwenye kutwaa eneo Lake hapo Tambaza kwa minajili ya upimaji/mipango miji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ