Panya Ronin amekuwa panya wa kwanza kugundua zaidi mabomu 100 ya kutegwa ardhini na mabaki mengine ya zana za kivita ambazo zinaweza kusababisha maafa nchini Colombia
Panya huyo mkubwa kutoka bara la Afrika amekuwa akifanya kazi katika jimbo la Preah Vihear kaskazini mwa Cmabodia kwa zaidi ya miaka mitatu.
Panya Ronin amenusa mabomu 109 ya ardhini nchini Cambodia, na kuvunja Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa mabomu mengi ya ardhini yaliyogunduliwa na panya.
-
Panya huyo mkubwa wa Kiafrika mwenye umri wa miaka 5 aliyetokea Tanzania pia amepata vipande 15 vya ziada vya silaha ambazo hazijalipuka (UXO) tangu alipopelekwa nchini Cambodia na shirika la APOPO.
Kwa zaidi ya miaka 25 shirika la Ubelgiji la APOPO limekuwa likifundisha panya wakubwa wa Kiafrika kunusa mabomu yaliyotegwa ardhini ambayo yaliachwa baada ya vita
APOPO wamekuwa wakishirikiana kwa karibu na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo nchini Tanzania ambapo panya wote huazaliwa na kufugwa huko.
Source: BBC News Swahili