Mfahamu Peter the Great, Mtawala mbabe aliyeibadilisha Russia

Mfahamu Peter the Great, Mtawala mbabe aliyeibadilisha Russia

Beberu

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2017
Posts
4,548
Reaction score
9,740
Nawasalimu katika jina la Kibepari

Peter the Great, ambaye jina lake kamili ni Peter I wa Urusi, alizaliwa tarehe 9 Juni 1672 (sawa na tarehe 30 Mei 1672 katika kalenda ya Juliasi) huko Moscow, Urusi na aliongoza urusi toka mwaka 1682-1721 kama Tsar wa urusi na kisha toka 1721 hadi 1725 kama Emperor wa Russia kubwa (Emperor of great Russia).

Peter the Great akiwa mtoto
Picha linaanza jamaa alianza kuwa Tsar of Russia (mtawala) akiwa na umri wa miaka 10 tu, hapo akiongoza na kaka yake wa kwa mama mwingine Ivan V (huyu Ivan alikuwa na matatizo mengi ya kiafya, alikuja kufa akiwa mdogo na ndo jamaa akawa sole owner)

Kipind hicho ana miaka 10 mama yake Natalya ndo alikuwa Regent, alikuja kuchukua full power toka kwa mama yake akiwa na miaka 22 baada ya mama yake kufariki.

Akiwa mdogo alionesha sana chachu ya kujifunza ujenzi wa meli (Shipbuilding) pamoja na mambo ya kijeshi na silaha ambayo ilikuwa ni kawaida kwa status yake.

Huyu jamaa baada ya kuingia madarakani alipenda sana kusafiri na kujionea mambo mengi ya nchi za nje (Exposure), alitembelea sana Uk, Dutch(waholanzi) Germany, Spain, kote huko aliona vitu vingi sana, aliona jinsi ambavyo Urusi imeachwa nyuma katika mambo mengi sanaaa, yeye alitamani urusi iwe sawa na nchi nyingine za Ulaya. (Western) alipenda sayansi, uhuru wa watu and the likes.

Sasa leo beberu nakuletea vitu vichache alivyovifanya huyu mwamba

#1.Mabadiliko ya Kijeshi: Peter the great aliimarisha jeshi la Urusi na kufanya mabadiliko makubwa ya kijeshi. Alileta mafundi wa kigeni na teknolojia mpya ili kuboresha jeshi la Urusi, na hapa alisafiri akwaleta wadutch wa Dutch East Limited, wamtengenezee silaha, wabuni uongozi mpya wa kijeshi, in short alifanya kama walivyofanya China, alikuwa anacopy na kupaste kutoka kwa westerners

Safari Peter the Great alifanya safari ya kujifunza katika nchi za Ulaya Magharibi ili kuchukua mafunzo na kuiga mifumo ya utawala na maendeleo ya viwanda. Alijifunza mambo mengi, kuanzia ujenzi wa meli hadi sanaa na sayansi jamaa alipenda sana kujifunza vitu vipya na kuvifanyia kazi.
In short jamaa alipenda sana kuzurula na kujifunza

Jiji Jipya: Peter the Great alihamishia makao makuu ya Urusi kutoka Moscow hadi St. Petersburg. Alitumia nguvu kubwa kujenga jiji jipya lenye usanifu wa kisasa, ambalo lilikuwa ishara ya mabadiliko ya Urusi kuelekea Ulaya, Japo baadae after WW2 makao makuu yalirudishwa Moscow ambako ndio makao makuu hadi sasa
Unaambiwa ile saint Petersburg ya leo ndo aliijenga jamaa kwa kufuata muundo wa majiji aliyoyaona huko alikoenda kutembelea, aliweka kila kitu kama ulaya, na ni kweli moja kati ya majiji mazuri St.Petersburg huwezi likosa
NB. Jina la mji halitokani na jina lake

Mfumo wa Utawala: Peter The Great aliboresha mfumo wa utawala wa Urusi kwa kuunda taasisi mpya na kuzingatia zaidi sheria na utawala bora. Alianzisha Baraza la Seneti na Baraza la Taasisi, ambazo zilisimamia shughuli za serikali.

Mabaraza haya yalikuja kuvunjwa miaka ya 1970s

Jeshi la Maji: Peter the great alijenga jeshi la maji lenye nguvu na kuunda Bahari Nyeusi na Bahari ya Baltiki kuwa vituo muhimu vya bahari kwa Urusi. Alitilia mkazo umuhimu wa Urusi katika siasa za kimataifa kupitia nguvu za bahari.

Na kupitia jeshi hilo akafanikiwa kuipiga Sweden, ambayo ilikuwa inasumbua sana eneo la Baltic miaka hio ya 1700s, licha ya kuwa ilimchukua majaribio kama matatu hiv + alipoteza wanajeshi wengi ila alishinda vita vile na hapo sasa watu wakaanza kumuona Russia kama moja ya wababe duniani

Elimu na Utamaduni: Peter The great alikuwa na hamu kubwa ya kukuza elimu na utamaduni nchini Urusi. Alianzisha Shule ya Sayansi na Chuo Kikuu cha St. Petersburg ili kuendeleza elimu ya juu na utafiti.

Chuo cha St.Petersburg ni chuo kikongwe zaidi Russia, na alikijenga baada ya kujifunza toka UK na Oxford yao
Pia yeye akaleta mfumo rasimi wa kwamba watoto wote wa viongozi wa serikali wanapaswa kwenda shule na kusoma rasmi, miaka hio watu wanajifunza tu kila mtu kivyake ila sasa ikawa ndo kama madarasa na ndo hivyo hadi chuo kikuu

Mfumo wa Kalenda: Peter the great alibadilisha kalenda ya Urusi kwa kufuata mfumo wa Gregorian ambao ulikuwa tayari umeanza kutumika Ulaya Magharibi. Hii ilileta Urusi katika mfumo sawa wa kalenda na nchi zingine za Ulaya.

Kipindi Peter anaibadili kalenda ya urusi ili ifuate kalenda ya kimagharibi ilikuwa mwaka 1692 na hapo kwa kalenda ya urusi ilikuwa mwaka 17900+, kipind hicho kalenda ya urusi ilikuwa based on mwaka wa kuundwa urusi wakati ile ya kimagharibi ilikuwa based na kuzaliwa kwa Yesu

Uchumi na Viwanda: Peter the great alifanya jitihada kubwa za kuimarisha uchumi na viwanda vya Urusi. Alifanya mageuzi ya kifedha, kuongeza biashara ya kimataifa, na kukuza viwanda vipya ili kuimarisha uchumi wa nchi.
Mtu aliependa kusoma sana, aliona uchumi unavyoenda, akajenga viwanda vingi sana Urusi, viwanda vya nguo, viwanda vya mitambo na vingine vingi, jamaa alikuwa akisafiri lazima aje na kitu kipya home

Mabadiliko ya Utamaduni: Peter the great alianzisha sera za kubadilisha utamaduni wa Kirusi ili kufanana zaidi na utamaduni wa Ulaya. Aliweka sheria zilizopiga marufuku ndevu nyingi kwa wanaume hapo kipind hicho urusi ndevu zilikuwa kama fashion hivi, watu wakawa kama mabeberu unamkuta mtu ana mdevu nyingiiiiiii, bas jamaa akapiga marafuku, watu wakalalamika sana, ikabidi aruhusu lakini kwa sharti la kuweka kodi ya ndevu 😂😂😂 watu walinyoa wenyewe dadeq 😂😂😂😂 ( Tuombe hii asiione Mwigulu, ataileta bongo )

Huyu jamaa ndio kawa credited na modernization ya Russia, alibadili mind za watu wa Russia kuwa more Western

Nb. Viongozi wetu kila siku wapo kwenye ziara za kujifunza kwenye mataifa ya watu ila matokeo tunayoyaona ni madogo sanaaaa, though yapo kama mfumo wa GePG, na mengineyo machache ila bado kwenye elimu, Afya, mpango miji bado tupo nyuma licha ya viongozi wetu kushinda nchi za nje wakijifunza mambo mbalimbali
 

Attachments

  • Young_Peter_the_Great_parsuna.jpg
    Young_Peter_the_Great_parsuna.jpg
    18.4 KB · Views: 6
  • download.jpeg
    download.jpeg
    6.8 KB · Views: 7
Back
Top Bottom