Mfahamu rafiki wa Wema anayedaiwa kumsaliti kwa kuanzisha uhusiano-na mwanaume aliyekuwa wa Wema

Mndengereko

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2011
Posts
7,296
Reaction score
3,398
Wazungu wanasema what goes around comes around. Picha linaanzaa miaka mtatu na kitu iliyopita, mitaa ya Mbagala jijini Dar es Salaam kwenye uchukuaji wa video ya wimbo wa pili wa Diamond uliompa mafanikio, Mbagala.

Katika scene ya mwisho pale Diamond anapoonekana kukaa chini akiwa amejiinamia kutokana na mawazo mengi aliyokuwa nayo kichwani, mara kama zali, anatokea msichana mrembo mwenye asili ya kiarabu akiwa amevalia gauni jekundu.

Kwa haraka haraka kama wewe ungekuwa Diamond, kwa urembo wa msichana huyo ni rahisi kuhisi labda ni malaika aliyeshuka juu kuja kuziondoa shida zako muda huo. Msichana huyo anakaa alipo Diamond na kumshika mikono kumaanisha kuwa angependa awe tulizo la moyo wake kwa muda huo. Wawili hao Wanainuka na kuondoka.

Msichana huyo anaitwa Naima Shaa aka J.LO, anayedaiwa kuwa mtoto wa mbunge, Abdulkarim Shaa wa Mafia.










Marehemu Sharo Milionea akiwa na Wema na NaimaLakini sasa meza zimebadilika. Kwa mujibu wa tetesi za mtaani na pia gazeti la Ijumaa Wikienda likiweka msititizo, ni kwamba Naima na aliyekuwa mpenzi wa Wema, anayefahamika kwa jina la Clement ni wapenzi. Clement ndiye aliyekuwa mwanaume nyuma ya maisha ya kifahari ya Wema aliyemnunulia magari yake, kumpa nyumba, kumfungulia ofisi (vitu ambavyo tayari inasemekana amenyang'anywa kutokana na Wema kuendeleza uhusiano wake na Diamond).


Kwa mujibu wa chanzo kinachodaiwa kuongea na gazeti hilo la udaku la kampuni ya Global Publishers, Clement ameamua kutembea na Naima ili kumuumiza roho Wema. "Unaambiwa nyuma ya pazia stori ni kwamba anataka Wema aumie ndiyo maana ameamua kubanjuka na Naima huku akijua kabisa kuwa ni marafiki," gazeti hilo limekinukuu chanzo hicho.Tayari kuna picha ya Naima inayomuonesha akiwa amejichora tattoo yenye jina la Clement.

"Naima naye amedata kabisa na sidhani kama anaogopa Wema kujua kama yeye ndiye hasa anatembea na kigogo huyo kwa kipindi hiki," chanzo hicho kilinukuliwa na gazeti hilo. Hata hivyo Naima amekanusha kwa kudai kuwa tattoo hiyo inamaanisha ‘Element' na sio ‘Clement'.Gazeti hilo linadai kuwa Wema haumizwi na wawili hao kuanzisha uhusiano kwakuwa tayari yupo na mtu anayempenda kwa dhati. "Moyo wangu ulishatulia kwa nimpendaye, nawatakia maisha mema," Wema anadaiwa kuliambia gazeti hilo.Kinachoifanya drama hii inoge, ni kwamba Naima naye ni mke wa mtu ambaye tayari ameingia kwenye mgogoro kwa kusaliti ndoa yake. "Unajua hata Naima ameingia kwenye gogoro la kindoa na mumewe kwa muda mrefu. Kisa ni huyo CK."

Picha zaidi za Naima












Maelezo ya ziada: Ijumaa Wikienda, Picha: Instagram
 
Last edited by a moderator:
Mi nasubir hvyo vifaa alivyoaidiwa wema na diamond kuwa haitapita hata wiki mbili atamnunulia...
 
jamani mwenye picha ya huyo clement ebu aniwekee na mie nimjue
 
Mi nasubir hvyo vifaa alivyoaidiwa wema na diamond kuwa haitapita hata wiki mbili atamnunulia...

Aisee hata mi nahesabu nadhani ishapita wikii nasubiri kwa hamu na ile nyumba atakayopangishiwaa watu na bahati zao sijui zao zina nini yarabi!!!!!!
 
Aisee hata mi nahesabu nadhani ishapita wikii nasubiri kwa hamu na ile nyumba atakayopangishiwaa watu na bahati zao sijui zao zina nini yarabi!!!!!!

Ukitaka utapata, lakini lazima uingie ktk matandao wa hawa mabinti, na uwe na quality kama zao, madalali wakujue, hawa ndiyo ma connector wazuri kwa wadau na warembo, ila simu yako itakuwa busy sana, itabidi utafute line rasmi kwa issue hizo, nyingine ibaki ya family na ndugu, ukiwa site line yao unazima au always ibaki silent!.
 
Aisee hata mi nahesabu nadhani ishapita wikii nasubiri kwa hamu na ile nyumba atakayopangishiwaa watu na bahati zao sijui zao zina nini yarabi!!!!!!

Wema hamnazo ,diamond mwenyewe nasikia analala kwenye nyumba ya clement,analalia kitanda cha clement,sasa yeye diamond kama Kidume si angempangishia Masaki au mbezi wakalale wote uko, wanajifanya wanamponda huk kitanda chake wanakojolea kila siku, shenz kabisa
 
Kumbe ndo huyu? Sasaivi kaja ofisini kwangu
Ni kweli mzuri me nimemuona live
kafuata nini ofisin kwako au na wewe unahusika na wasanii? nasanaaa? sasa si ungejitahidi upate walau na. ya simu?'
 
kafuata nini ofisin kwako au na wewe unahusika na wasanii? nasanaaa? sasa si ungejitahidi upate walau na. ya simu?'

Hapana mkuu kaja kama mtu wakawaida alitaka huduma yetu na wala sio mambo ya usanii
 
Wadada wa mjini wanakaziii....na huyo clement anaibisha civil servants wenzie...kwani hakuna kamati za maadili kukanyana...au afanye kimya kimya
 
Aisee hata mi nahesabu nadhani ishapita wikii nasubiri kwa hamu na ile nyumba atakayopangishiwaa watu na bahati zao sijui zao zina nini yarabi!!!!!!

Zimepita kwa babu, mtembezee tu aitie kwenye orodha!
 
Mtamaliza maduka, Nyama ni ile ile tu. Ukiila Sinza, Magomeni, au Gongo la Mboto. Ladha ile ile.
 

Domo nae ashazoea kuhongwaa ndio maana anaona Kawaidaa wala hashtuki mwanaume mwenye akili zake lazima atastukaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…