Mfahamu Rapper DMX

Mfahamu Rapper DMX

tc_edo

Senior Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
123
Reaction score
98
Earl Simmons ajulikanaye kama DMX alizaliwa tarehe 18 December 1970 huko Mount Vernon, New York, Marekani.

Wazazi wa Earl Simmons (DMX); Arnett Simmons na Joe barker walijaliwa kumpata mwanao wakiwa na miaka 19 (mama) na 18 (baba).

Alikua wa pili kuzaliwa katika familia ya watoto watano[emoji1284]; Bonita dada yake mkubwa, Shayla dada yake mdogo na wadogo zake wa kiume wawili. Baba wa Earl Simmons (DMX) alikua mchoraji alietumia rangi za maji kuchora maeneo mbalimbali ya mitaa na kuuza izo picha lakini baada ya huyu mzee kuhamia Philadelphia hakujihusisha sana na maisha ya wanae wala mkewe.

Earl Simmons (DMX) hakua na maisha mazuri katika ukuaji wake maana alipitia changamoto na misukosuko mingi katika maisha yake.

Alisumbuliwa sana na tatizo la upumuaji (Asthma) lililopelekea apelekwe mara kwa mara hospitalini. Alipokua na miaka sita alipigwa na mfagio na kutolewa meno mawili na mama yake. Pia shuleni alimchoma usoni mwanafunzi mwenzake na penseli[emoji51][emoji51].

Akiwa na miaka 10 alifukuzwa shule na kupelekwa katika kituo cha Julia Dyckman Andrus Children's Home kwa miezi 18, kituo hiki kilelea watoto wapitiao changamoto mbalimbali, mama yake alimrubuni kwa kumwambia wanatembelea sehemu hio na badala yake akamwandikisha na kumwacha uko kwa miezi 18 [emoji3064].

Miezi kadhaa baadae alikamatwa kwa kosa la kujaribu kuchoma shule. Alianza kuishi mitaani uko Yonkers hayo yote ilikua ni kukimbia unyanyasaji wa mama yake na alikua akilala katika kontena za kuombea nguo kwa ajili ya watu wenye shida mbalimbali, kontena hizi zilimilikiwa na kanisa la The salvation army (TSA).

Muda mfupi baada ya mama yake kugundua hili alimrudisha katika kituo cha kulelea watu wenye shida mbalimbali kiafya na watoto wasoweza kuishi na familia zao au wasio na kipato kuishi wenyewe (Group homes). Alikutana na vijana wenzake waliovutiwa na muziki wa hip hop na waliomhimiza Earl Simmons (DMX) kuandika nyimbo.

Ⓣⓞ ⓑⓔ ⓒⓞⓝⓣⓘⓝⓤⓔⓓ...... [emoji6]

1618909007840.png
 
Asante kwa taarifa mku japo nilichelewa
 
ⓀⓊⓏⒶⓁⒾⓌⒶ

Earl Simmons ajulikanaye kama DMX alizaliwa tarehe 18 December 1970 huko Mount Vernon, New York, Marekani.

Wazazi wa Earl Simmons (DMX); Arnett Simmons na Joe barker walijaliwa kumpata mwanao wakiwa na miaka
Hizi ndio hussle sasa. Endelea mkuu sio wa huku jf eti alizamia chato
 
Back
Top Bottom